Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacha wa Pacome Zouzoua aweka rekodi Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Huku pia akiondoka uwanjani kama Mchezaji Bora wa Mechi (Player of the Match) katika ushindi wa bao 1-0 ambao Ivory Coast imeupata usiku wa kuamkia leo, Jumatatu dhidi ya Ecuador.

WINGA Yan Diomande ambaye kwa mara ya kwanza aliitwa na kucheza sambamba na Pacome Zouzoua wa Yanga, ameweka historia mpya kwenye Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuichezea Ivory Coast katika mashindano hayo makubwa.

Huku pia akiondoka uwanjani kama Mchezaji Bora wa Mechi (Player of the Match) katika ushindi wa bao 1-0 ambao Ivory Coast imeupata usiku wa kuamkia leo, Jumatatu dhidi ya Ecuador.

Diomande, anayekipiga RB Leipzig ya Ujerumani, alionesha kiwango bora, akidhibiti kasi ya mchezo na kuwa tishio katika safu ya ushambuliaji ya  Ivory Coast.

Rekodi yake sasa inamweka rasmi kama mchezaji mwenye umri mdogo zaidi akiwa na miaka 19 kuichezea Ivory Coast katika Kombe la Dunia.

Oktoba 10,2025 winga huyo aliichezea kwa mara ya kwanza Ivory Coast sambamba na nyota wa Yanga Pacome katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.

Winga moja alikuwa Diomande huku kwingine akiwa Pacome, wawili hao waliisaidie Ivory Coast kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 na huo ndio ukawa mwanzo wa kinda huyo kuendelea kuaminiwa.

Alifunga na kutoa asisti moja kabla ya Ivory Coast kufuzu kwa mara ya  nne kucheza fainali hizo za Kombe la Dunia.

Kwenye klabu yake ya RB Leipzig, Diomande amekuwa mmoja wa vijana wanaofanya vizuri Ulaya.

Msimu wake wa kwanza uliisha akiwa na mchango wa moja kwa moja kwenye mabao 22, ambapo alifunga mabao 13 na kutoa asisti 9 katika mashindano yote ya klabu hiyo ya Bundesliga.

Takwimu hizo zimekuwa msingi wa kuaminiwa kwake hata katika timu ya taifa, ambapo sasa ameanza kujijengea jina kama mmoja wa nyota chipukizi wanaoweza kuibeba Ivory Coast katika miaka ijayo.