Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oxlade-Chamberlain bado kidogo asepe zake huko

OX Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa England amekuwa kwenye mazungumzo na klabu hiyo ya Uturuki kuvunja mkataba wake ili awe mchezaji huru.

ISTANBUL, UTURUKI: STAA, Alex Oxlade-Chamberlain yupo kwenye hatua za mwisho za kuachana na Besiktas ya Uturuki.

Kiungo huyo wa zamani wa England amekuwa kwenye mazungumzo na klabu hiyo ya Uturuki kuvunja mkataba wake ili awe mchezaji huru.

Na sasa, hilo linaonekana kwenda kutimia kwa Oxlade-Chamberlain, 31, ambaye amekuwa akifanya mazoezi kwenye kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer yenye maskani yake Istanbul.

Aliondoka Liverpool mwaka 2023 na bado ana mkataba na Besiktas hadi mwaka 2026. Lakini, amekuwa kwenye wakati mgumu wa kupata kiwango chake bora.

Oxlade-Chamberlain amefunga mabao matano na kuasisti moja tu katika mechi 50 alizoichezea Besiktas. Na staa huyo wa zamani wa Arsenal na Southampton sasa ana matumaini kibao ya kurudi kwenye Ligi Kuu England.

Leeds United inatazamwa kama timu ambayo kiungo anaweza kujiunga nayo.