Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oklahoma City Thunder yabeba ubingwa NBA 2025

OKLOHAMA Pict

Muktasari:

  • Thunder ilionekana iko tayari tangu dakika ya kwanza ikiongozwa na Shai Gilgeous-Alexander aliyekuwa moto wa kuotea mbali,  akifunga pointi 29 na kuisaidia timu yake kuweka mwanya wa mapema ambao Pacers ilishindwa kuufidia.

OKLAHOMA, MAREKANI: Oklahoma City Thunder imeandika historia kwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), baada ya kuichapa Indiana Pacers kwa pointi 103-91 katika mchezo wa saba  (Game 7) ya fainali, ikimaliza mfululizo wa mechi saba kwa ushindi wa 4-3.

Thunder ilionekana iko tayari tangu dakika ya kwanza ikiongozwa na Shai Gilgeous-Alexander aliyekuwa moto wa kuotea mbali,  akifunga pointi 29 na kuisaidia timu yake kuweka mwanya wa mapema ambao Pacers ilishindwa kuufidia.

Indiana Pacers ilijitahidi kurudi mchezoni katika robo ya pili kwa kuongozwa na Bennedict Mathurin  aliyefunga 24, lakini ukuta wa Thunder ulikuwa mgumu kupenya, huku Josh Giddey na Jalen Williams wakitoa mchango mkubwa kwenye ulinzi.

Game 7 ilikuwa ni onyesho la umahiri wa kikosi cha vijana cha Thunder kilichojengwa na kujengeka, ikionyesha ukomavu mkubwa licha ya kutokuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu wa fainali kama Pacers.

Katika robo ya tatu, Thunder walizidi kuwakamata Pacers kwa mashambulizi ya nguvu na kufunga mfululizo wa pointi 12 bila jibu, jambo lililowavunja nguvu wapinzani na kuwafanya waone mchezo ukielekea kupinduka.

Ushindi huo unaifanya Thunder kuwa miongoni mwa timu chache zilizoibuka na taji la NBA kupitia mpango wa muda mrefu wa kuwatengeneza vijana ndani ya klabu bila kutegemea mastaa wa bei ghali kutoka nje.

MVP wa fainali hiyo alikuwa Shai Gilgeous-Alexander, ambaye mchango wake katika kila mchezo wa fainali ulikuwa dhahiri si tu kwa pointi, bali kwa uongozi, maamuzi ya haraka na kutengeneza nafasi kwa wengine.

Indiana Pacers, licha ya kushindwa, walionyesha ujasiri mkubwa katika mfululizo mzima wa fainali, na wachambuzi wengi wamewapongeza kwa safari yao ya ajabu kufikia hatua hiyo, wakitarajiwa kuwa tishio kubwa katika misimu ijayo.

Taji hilo ni la pili kwa Oklahoma City tangu walipoingia NBA, na linaashiria mwanzo wa enzi mpya ya mafanikio kwa kikosi hicho kinachoonekana kuwa na msingi thabiti wa mafanikio ya muda mrefu.