Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Aston Villa alizwa mimba kutoka

NYOTA Pict

Muktasari:

  • Kabla ya habari hii ya kusikitisha, Kearns aliomba kuwa nje ya majukumu yake kwa kipindi kilichosalia kwa msimu kutokana na ujauzito aliobeba.

LONDON, ENGLAND: NYOTA wa timu ya taifa la England, Bo Kearns kwa upande wa wanawake, amefichua kupoteza mtoto, ikiwa ni wiki chache baada ya kutangaza mjazito.

Mchezaji huyo wa Aston Villa alieleza kwamba yeye na mpenzi wake ambaye naye ni mchezaji, Liam Walsh wa Luton Town walikuwa wakitegemea mtoto wao wa kwanza lakini kwa huzuni Kearns alitumia mtandao wa kijamii wa Instagram Jumapili kufichua kwamba ujauzito huo umetoka.

“Kwa mioyo mizito sana, tunataka kueleza kwamba tumepoteza mtoto wetu wakati wa ujauzito,” amesema na kuongeza:

“Katika wiki zilizopita tumekuwa na huzuni isiyoelezeka na bado tunajaribu kuikubali hali iliyotokea kwa sasa tunazingatia kuwa sawa kutokana na kilichotokea, tunashukuru sana kwa upendo na msaada ulio karibu nasi zaidi ya tunavyoweza kueleza.”

Mwanzoni mwa mwezi huu, Kearns 24 alitangaza kuwa na ujauzito kupitia video ambapo alichora neno “Mum” (Mama) kwenye ukuta na Walsh baadaye kuongeza “Dad” (Baba).

Wapenzi hao walifichua kwamba mtoto wao angezaliwa mwezi Septemba huku Kearns akionyesha picha za uchunguzi wa mtoto (baby scans).

Kabla ya habari hii ya kusikitisha, Kearns aliomba kuwa nje ya majukumu yake kwa kipindi kilichosalia kwa msimu kutokana na ujauzito aliobeba.