Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nusu fainali Kombe la FA siyo kinyonge

FA Pict

Muktasari:

  • Manchester City ilitinga hatua hii baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool, wakati Southampton ikifuzu baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal.

LONDON, ENGLAND: DROO ya nusu fainali ya Kombe la FA imetoa picha mpya ya michuano hiyo kati ya timu zilizofuzu, huku kila moja ikipania kutinga fainali na hatimaye kutwaa ubingwa.

Katika droo hiyo, Manchester City itakutana na Southampton, huku Chelsea ikipangwa kucheza dhidi ya Leeds United.

Manchester City ilitinga hatua hii baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool, wakati Southampton ikifuzu baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal.

Kwa upande wa Chelsea, ilijihakikishia nafasi ya nusu fainali kwa kuichapa Port Vale mabao 7-0, huku Leeds United ikisonga mbele ikiitoa West Ham United kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida na wa nyongeza.

F 01

Michezo za nusu fainali zinatarajiwa kuchezwa Aprili 25 na 26 mwaka huu kwenye Dimba la Wembley jijini London, huku kukiwa na matarajio makubwa ya mechi kali zitakazoamua nani ataingia fainali.


SASA ITAKUWAJE

Leeds United itamenyana na Chelsea ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika nusu fainali ya FA Cup ndani ya miaka 39.

Chelsea iliweka pembeni changamoto zake za ligi na kuifunga Port Vale mabao 7-0, ambapo wachezaji sita tofauti wa kikosi hicho walifunga mabao hayo ambao ni Jorrel Hato (dk 2), João Pedro (dk 25), Tosin Adarabioyo (dk 57), Andrey Santos (dk 69), Estêvão (dk 82) na Alejandro Gamacho (dk 90+2) kwa penalti, huku Jordan Lawrence-Gabriel akijifunga dakika ya 43.

F 02

Manchester City, iliyopoteza fainali ya FA Cup msimu uliopita dhidi ya Crystal Palace, sasa imepangwa kucheza na Southampton, timu ambayo iliwashangaza vinara wa Premier League, Arsenal, kwa ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa St Mary’s.

Viktor Gyokeres alisawazisha bao la awali la Ross Stewart, kabla ya Shea Charles kufunga bao la ushindi dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo huo.

Sasa Southampton inakwenda kukutana na Manchester City, ambayo imeshawahi kutwaa kombe hilo mara saba, wakati wenyewe wametwaa mara moja tu mwaka 1976 walipoifunga Manchester United kwa bao 1-0, fainali iliyochezwa Wembley.

F 03

Leeds United imefika nusu fainali mara ya mwisho mwaka 1987, ilipofungwa na mabingwa wa mwaka huo, Coventry City. Kombe lao pekee la FA Cup walilitwaa mwaka 1972.


NANI ANA NAFASI

Kabla ya kutupwa nje ya michuano hii, Arsenal walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali na pengine hata kwenda kubeba ubingwa, lakini sasa Manchester City inapewa nafasi kubwa ya kuwa bingwa baada ya kufuzu nusu fainali kwa msimu wa nane mfululizo.

City waliifumua Exeter City kwa mabao 10-1 katika raundi ya tatu, wakaifunga Salford City mabao 2-0 raundi ya nne, kisha wakageuza matokeo na kushinda 3-1 dhidi ya Newcastle United.

F 04

Kikosi cha kocha Pep Guardiola kina nafasi ya kutwaa mataji yote mawili makubwa ndani ya England, baada ya kushinda fainali ya EFL Cup dhidi ya Arsenal Machi 22, mwaka huu ambapo Nico O’Reilly alifunga mabao mawili ya vichwa ndani ya dakika tano za kipindi cha pili.

Chelsea ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi kati ya zilizosalia kwenye mashindano haya, ikiwa imeshatwaa kombe hilo mara nane.

Chini ya kocha Liam Rosenior, Chelsea wameonyesha kiwango bora katika mechi za ugenini, wakianza kwa kuichapa Charlton Athletic mabao 5-1, kisha Hull City mabao 4-0.

Baadaye walijikuta katika wakati mgumu dhidi ya Wrexham, lakini walishinda 4-2 baada ya muda wa nyongeza, kabla ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Port Vale.

Leeds United wanaonekana kuwa washindani wa tatu kwa ubashiri, huku Southampton, ambao pia waliwahi kushinda dhidi ya Fulham katika raundi ya tano, wakitajwa kama timu yenye nafasi ndogo zaidi.

Ikumbukwe kuwa, fainali ya mashindano haya itachezwa Jumamosi ya Mei 16, 2026 kwenye Uwanja wa Wembley.