Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nicol amtema Slot, ‘ampigia debe’ Alonso Liverpool

SLOT Pict

Muktasari:

  • Sasa macho na masikio ya mashabiki wa Liverpool yako kwa uongozi wa klabu hiyo kuona kama watafanya uamuzi mkubwa wa kubadilisha benchi la ufundi kabla ya msimu ujao kuanza.

LIVERPOOL, ENGLAND: NGULI wa zamani wa Liverpool, Steve Nicol amebadili msimamo wake kuhusu mustakabali wa benchi la ufundi la klabu hiyo na sasa anamtaka Xabi Alonso kuchukua nafasi ya Arne Slot.

Nicol, aliyewahi kushinda mataji manne ya ligi na Kombe la Ulaya akiwa Liverpool miaka ya 1980, awali alimtetea Slot akisema anastahili kupewa muda zaidi kurekebisha makosa ya timu hiyo, hasa baada ya mafanikio ya msimu uliopita. Hata hivyo, kipigo kizito cha mabao 4-0 walichopata Liverpool dhidi ya Manchester City katika Kombe la FA kimebadilisha mawazo yake.

Akizungumza na ESPN, Nicol amesema kutokana na chaguo zilizopo sokoni, Alonso ndiye anayefaa zaidi kuchukua mikoba hiyo.

“Kwa sasa, ukiangalia nani yupo sokoni, nadhani ningemchagua Alonso. Hakuna mwingine wa kiwango hicho,” amesema Nicol.

Aliongeza hapo awali alikuwa anaamini Slot ndiye mtu sahihi, lakini hali ya timu ilivyo sasa inaonyesha huenda mabadiliko yanahitajika. “Kiwango cha uchezaji ndicho kinachonifanya nifikirie upya,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Alonso ambaye aliwahi kuitumikia Liverpool kama mchezaji na kuacha alama kubwa, bado anaungwa mkono na mashabiki wengi wa timu hiyo. Wakati Liverpool wakiondoka uwanjani Etihad baada ya kipigo, baadhi ya mashabiki walionekana kuimba jina lake wakimtaka arejee klabuni hapo kama kocha.

Licha ya kuondoka mapema katika klabu yake ya awali, uzoefu wake kama kocha nchini Ujerumani umeongeza hadhi yake na kumfanya kuwa chaguo kuu endapo Liverpool itaamua kumtimua Slot.

Sasa macho na masikio ya mashabiki wa Liverpool yako kwa uongozi wa klabu hiyo kuona kama watafanya uamuzi mkubwa wa kubadilisha benchi la ufundi kabla ya msimu ujao kuanza.