Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki West Ham wamshambulia David Sullivan

SULLIVAN Pict

Muktasari:

  • Mashabiki waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa London waliimba nyimbo za kumkejeli Sullivan, jambo lililomfanya  kuondoka mapema kwenye jukwaa la viongozi wakuu kabla ya mechi kuisha. 

LONDON, ENGLAND: Mashabiki wenye hasira wa West Ham United wamemgeukia mmiliki mwenza wa klabu hiyo, David Sullivan, baada ya timu hiyo kushuka Ligi Kuu England hadi Championship.
 
Mashabiki waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa London waliimba nyimbo za kumkejeli Sullivan, jambo lililomfanya  kuondoka mapema kwenye jukwaa la viongozi wakuu kabla ya mechi kuisha. 

Sullivan na aliyekuwa makamu wake, Karren Brady, wamekuwa wakikabiliwa na maandamano kutoka kwa mashabiki msimu mzima.

SULL 01

                                                                                                                  Licha ya West Ham kupata ushindi dhidi ya Leeds katika mchezo wa mwisho, bado walihitaji Tottenham ifungwe na Everton ili kujinusuru, jambo ambalo halikutokea. 

Nahodha wa timu hiyo, Jarrod Bowen mwenye umri wa miaka 29, ameeleza kusikitishwa kwake na matokeo hayo akisema ni wakati mgumu sana kwa klabu kubwa kama hiyo kushuka daraja. 

SULL 02

Bowen ameongeza kuwa japo kuna tetesi za yeye kuhitajika na Chelsea na Newcastle, lengo lake kwa sasa ni kuisaidia timu hiyo kurejea Premier League, ingawa klabu inalazimika kuuza wachezaji ili kupata zaidi ya Pauni milioni 100 kufuatia anguko hilo.

Kwa upande mwingine, kocha Nuno Espirito Santo amewaomba msamaha mashabiki na kueleza kuwa ulikuwa msimu wa ajabu kwani pointi 39 walizovuna hazikutosha kuwabakiza ligi kuu. 

SULL 03

Licha ya uongozi wa West Ham kutaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 abaki klabuni hapo, inasemekana anapanga kuondoka. Nuno amesisitiza kuwa jambo la muhimu kwa sasa ni klabu hiyo kupita katika kipindi hiki cha huzuni na kujipanga upya ili kurudi haraka kwenye ligi kuu ya England.