Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

No Champions League, no Gyokeres Man United

Man Utd Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa kimataifa wa Sweden, Gyokeres, 26, amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Old Trafford kwa miezi kadhaa na haionekani kuwa ni kitu cha ajabu kwa kocha Ruben Amorim, ambaye alifanya kazi na straika huyo huko Sporting Lisbon kumtaka wakaungane tena Man United.

MANCHESTER,  ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Manchester United ipo kwenye hatari ya kukosa huduma ya straika Viktor Gyokeres kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya mkali huyo kutaka dili la kwenda kujiunga na timu itakayompa fursa ya kucheza soka la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Staa huyo wa kimataifa wa Sweden, Gyokeres, 26, amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Old Trafford kwa miezi kadhaa na haionekani kuwa ni kitu cha ajabu kwa kocha Ruben Amorim, ambaye alifanya kazi na straika huyo huko Sporting Lisbon kumtaka wakaungane tena Man United.

Man United imekuwa na ukame wa mabao msimu huu kutokana na mastraika wake Rasmus Hojlund na Joshua Zirkzee kushindwa kufanya kweli, licha ya kwamba mpango wa kumnasa Gyokeres kwenye dirisha lijalo utawahakikishia mabao.

Ripoti zinafichua kwamba Gyokeres bado yupo kwenye rada za Man United, lakini shida mchezaji mwenyewe anataka kucheza timu itakayompa nafasi ya kukipiga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kitu ambacho kinafanya Man United kijasho kuwatoka kwa sasa.

Man United inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi msimu huu, huku tayari theluthi mbili ya mechi za msimu huu zimeshachezwa. Na hata kama kikosi hicho cha Amorim kitapindua meza na kupata, kumaliza kwenye Top Four ni kitu kigumu kwao.

Matumaini pekee ya Man United ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya yapo kwenye ushindi wa ubingwa wa Europa League, kitu ambacho ni rahisi kusema kuliko kufanya, ambapo sasa kwenye hatua ya mtoano imechezesha mechi ya kwanza kwenye sare ya 1-1 na Real Madrid ikisubiri kurudiana wiki ijayo.

Wakati matumaini ya Man United kumnasa Gyokeres yakionekana kuwa kwenye mushkeri mkubwa, staa huyo mpango wake ni kuachana na Sporting Lisbon kwenye dirisha lijalo na saini yake inasakwa kwelikweli baada ya kufunga mabao 37 katika mechi 39 alizochezea klabu yake msimu huu.

Ripoti zilifichua kwamba staa wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta naye yupo kwenye rada za Man United. Fowadi huyo Mfaransa anaripotiwa kuwa na vigezo vyote vinavyotakiwa, vya kwenda kucheza kama mshambuliaji pekee kwenye fomesheni ya kocha 3-4-3, ambapo kuna wakati inakuwa 3-4-2-1.

Mastraika wengine ambao Man United inaweza kuhangaika kufukuzia huduma zao kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi ni Benjamin Sesko wa RB Leipzig na Liam Delap wa Ipswich Town.