Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne zatajwa kuitaka saini ya Robertson

ROBERTSON Pict

Muktasari:

  • Robertson ameisaidia Liverpool kushinda mataji kadhaa yakiwemo mawili ya Ligi Kuu England, moja Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya Carabao, moja la FA pamoja na Kombe la Dunia la Klabu, UEFA Super Cup na Ngao ya Jamii England.

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa kushoto wa kimataifa wa Scotland, Andrew Robertson, amethibitisha kuwa ataondoka Liverpool mwisho wa msimu huu baada ya miaka tisa kwenye Uwanja wa Anfield, lakini tayari kuna klabu nne zinazowania saini yake.

Robertson ameisaidia Liverpool kushinda mataji kadhaa yakiwemo mawili ya Ligi Kuu England, moja Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya Carabao, moja la FA pamoja na Kombe la Dunia la Klabu, UEFA Super Cup na Ngao ya Jamii England.

Hata hivyo, amekuwa akicheza kwa nadra msimu huu baada ya ujio wa Milos Kerkez, na taarifa zinaeleza kuwa klabu nne zinaongoza kumtaka msimu ujao.

The Star inaripoti kuwa, Tottenham Hotspur waliokuwa karibu kumsajili Januari, mwaka huu, lakini mpango ukavunjika dakika za mwisho wamemrudia tena safari hii wakimtaka akiwa nchezaji huru. Hata hivyo, mustakabali wao katika Ligi Kuu England unaweza kuathiri uamuzi wake, hasa iwapo klabu hiyo itashuka daraja kwenda EFL Championship.

Kwa upande mwingine chini ya kocha Diego Simeone, Atletico Madrid walijaribu kumsajili majira ya joto yaliyopita, lakini wakakwama na mara hii wamechomoza tena. Timu hiyo tayari imefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya  msimu ujao na inahitaji uzoefu wa Robertson.

Nayo Juventus imekuwa ikisajili wachezaji wakongwe kwa mafanikio imebisha hodi, na licha ya Andrea Cambiaso kuwa ndiye beki wa kushoto wa kudumu, lakini uzoefu wa Robertson unaweza kuisaidia klabu hiyo kurejea kileleni mwa Serie A.

Mbali na timu hizo tatu, Napoli, chini ya Antonio Conte, ipo kwenye mbio za ubingwa wa Serie A imewasiliana moja kwa moja na mchezaji huyo, kwani mfumo wa mabeki watano wa kocha huyo unaweza kumhusisha pia Robertson, ambaye amewahi kucheza kama 'wing-back'. Pia, kuhamia Naples kunaweza kumpa nafasi ya kushinda mataji zaidi.