Nketiah bado kidogo

New Content Item (1)
New Content Item (1)

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri Eddie Nketiah bado anaendelea kuvaa kifaa maalumu ambacho kinamsaidia kulinda mguu wake baada ya kuumia goti.

Nketiah amekosa mechi tatu za mwisho za Arsenal kutokana na jeraha la goti linalomsumbua, hadi tunaingia mtamboni aliukosa mchezo wa marudiano wa raundi ya 16 bora ya Ligi ya Europa dhidi ya Sporting Lisbon.

Straika huyo alionyesha kiwango bora alipopewa nafasi na Arteta baada ya Gabriel Jesus kuwa nje ya dimba. Sasa Nketiah hatajumuishwa kikosi kwa muda wiki kadhaa.
Arteta ana matumaini Nketiah angerejea dimbani baada ya mechi za kimataifa lakini wataangalia kama atakuwa fiti asilimia 100.

"Anaendelea vizuri. Bado anaendelea kuvaa kifaa cha kumlinda mguuni, bado ana amebakiza wiki kadhaa tunachotakiwa tuwe na subira, aliumia vibaya na ana ushindani mkubwa mbele yake, tunashukuru kila kitu kimeenda sawa, naamini Nketiah atarudi tusubiri," alisema Arteta

Arsenal ilipata ahueni baada ya Gabriel Jesus aliporejea dimbani kwa mara ya kwanza dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita, hata hivyo fowadi huyo wa kimataifa wa Brazil bado hajawa fiti asilimia 100 lakini kurejea kwake kikosini kumempa matumaini Arteta.

"Nimefurahi kumuona Jesus kila mtu alichekelea, wachezaji na benchi la ufundi, tunachotakiwa ni kuwa makini na dakika anatakazocheza. Anajisikia vizuri kila siku na anafanya mazoezi na wenzake," aliongeza