Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nigeria, Misri kucheza mechi ya kirafiki leo

MISRI Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo itapapatuana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo nchini Misri saa 3:00 usiku wa kwa saa za Afrika mashariki.

Timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, itashuka dimbani leo Jumanne, Desemba 16, 2025 kuivaa timu ya taifa ya Misri, Pharaohs katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. 

Miamba hiyo itapapatuana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo nchini Misri saa 3:00 usiku wa kwa saa za Afrika mashariki.

Timu za mataifa hayo mawili zimeweka kambi nchini Misri na zitaitumia mechi ya leo kujaribu wachezaji wapya pamoja na mbinu tofauti za kiufundi kabla ya kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025, Desemba 21 mwaka huu. 

MISR 01

Kocha mkuu wa Nigeria, Eric Chelle, amewajumuisha baadhi ya wachezaji wapya kwenye kikosi chake, akiwemo Ebenezer Akinsanmiro, Usman Mohammed, Tochukwu Nnadi, Ryan Alebiosu na Salim Fago Lawal.

Wachezaji hao wanatarajiwa kupata nafasi ya kucheza dhidi ya Misri, mechi ambayo pia ni fursa muhimu kwa baadhi ya wachezaji kuthibitisha uwezo wao na kujihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Super Eagles.

Kwa sasa, wachezaji 22 wa Nigeria tayari wamewasili na kuweka kambi katika Hoteli ya Renaissance iliyopo Cairo. Hata hivyo, mastaa kadhaa akiwemo Victor Osimhen, Moses Simon na Samuel Chukwueze wanatarajiwa kuungana na kikosi hicho baadaye nchini Morocco.

Nigeria imepangwa Kundi C kwenye mashindano ya AFCON 2025 sambamba timu za Tunisia, Uganda na Tanzania, ambapo kila timu itacheza mechi tatu za hatua ya makundi kupigania nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora.

Katika michuano hiyo, Super Eagles itaanza kampeni yake kwa kuikabili Tanzania Desemba 23. Baada ya hapo, Desemba 27 Nigeria itacheza dhidi ya Tunisia. Mechi ya mwisho ya hatua ya makundi kwa Nigeria itakuwa dhidi ya Uganda, Desemba 30.

MISR 02

Kwa upande wa Misri, imepangwa Kundi B sambamba na timu Afrika Kusini, Angola na Zimbabwe.

Mechi za Misri katika hatua ya makundi zitaanza Desemba 22, ambapo itacheza dhidi ya Zimbabwe. Baadaye, Desemba 26, itakutana na Afrika Kusini katika pambano lililotarajiwa kuwa gumu kwani pande zote mbili zinataka nafasi ya juu kwenye kundi hilo. 

Mechi ya mwisho ya kundi itakuwa dhidi ya Angola, Desemba 29, 2025, ambapo Misri itajaribu kuhakikisha inamaliza hatua ya makundi kwa matokeo mazuri ili kupata nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano.