Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nicky Butt awekwa kwenye kona, kulipa fidia ya mamilioni

BUTTY Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo aliyewahi kutamba na Manchester United mwenye umri wa miaka 50, tayari amefunguliwa mashtaka na mpanda pikipiki, Adam Fielding, ambaye alipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu.

NYOTA wa zamani wa England, Nicky Butt, huenda akalipa maelfu ya pauni kama fidia baada ya kumgonga mtu aliyekuwa anaendesha pikipiki na kumvunja mguu.

Mchezaji huyo aliyewahi kutamba na Manchester United mwenye umri wa miaka 50, tayari amefunguliwa mashtaka na mpanda pikipiki, Adam Fielding, ambaye alipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu.

Butt, akiwa kwenye gari aina ya Range Rover, alitoka kwenye makutano bila tahadhari na kumgonga Fielding aliyekuwa akiendesha pikipiki ya Honda huko Burnley, Oktoba 2022.

Mwaka 2024, Butt alikiri kosa la kuendesha gari kwa uzembe, hali iliyopelekea kumgonga Fielding na kumsababishia majeraha makubwa, huku akipigwa marufuku kuendesha gari kwa mwaka mmoja na mahakama ya Blackburn.

BUT 01

Sasa anakabiliwa na kesi ya madai ya kiraia na Fielding, mwenye umri wa miaka 29, ambaye aliwahi kueleza amekuwa akiishi kwa maumivu makali kwa takriban miaka miwili sasa.

Alipewa matibabu hospitalini kwa wiki mbili baada ya kuvunjika mguu wa kushoto na alifanyiwa upasuaji wa kuwekwa vyuma.

Ajali hiyo ilisababisha apoteze kazi yake ambayo ilikuwa ya kutumia nguvu nyingi, akaathiri maisha yake ya kijamii, na hata uhusiano wake wa kimapenzi kubadilika kwani mpenzi wake aligeuka kuwa mlezi wake.

Fielding, aliyekuwa akifanya kazi Screwfix, anawakilishwa na kampuni ya wanasheria wa majeraha binafsi ya Minster Law.

Haijafahamika ni kiasi gani Butt anaweza kuamuliwa kulipa kama fidia. Hata hivyo ameomba msamaha na amesema ajali hiyo inamsumbua mawazoni kila siku.

BUT 02

Nyaraka za Mahakama Kuu zilizoonwa na gazeti la The Sun zinaonyesha pande mbili hizo zinatofautiana kuhusu baadhi ya ukweli wa tukio hilo.

Waathirika wa ajali huwa na miaka mitatu kufungua madai ya kiraia, hivyo Fielding amewasilisha kesi yake wiki chache kabla ya muda kuisha.

Jaji atalazimika kutoa uamuzi kabla ya kesi ya madai kusikilizwa, ikiwemo iwapo Butt atawajibika kulipa fidia.

Iwapo Butt atashindwa kesi hiyo, inadhaniwa kuwa kampuni yake ya bima ndiyo italipa fidia kwa Fielding, kama ilivyo kawaida katika kesi nyingi za ajali.