Neymar mchezaji bora wa Amerika Kusini

Mshambuliaji chipukizi Brazil, Neymar
MONTEVIDEO, Uruguay MSHAMBULIAJI chipukizi Brazil, Neymar ametajwa mchezaji bora wa mwaka wa Amerika Kusini baada ya kuisaidia klabu yake ya Santos kutwaa taji la Copa Libertadores. Kocha wa Uruguay,Oscar Washington Tabarez ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa mara ya pili baada ya kuiongoza nchi hiyo kufika nusu fainalia ya Kombe la Dunia pamoja na kutwaa taji la 15 la Copa Amerika mwezi Julai. Neymar, aliiongozaa Santos kushinda dhidi ya Penarol ya Uruguay kwenye fainali ya Copa Libertadores iliyofanyika mwezi Juni, alimpokea taji hilo kiungo wa Argentina, Andres D’Alessandro anayechezea klabu ya Brazil, Internacional aliyetwaa taji hilo mwaka jana, kwenye kura zilizoendeshwa Amerika Kusini na jarida la Uruguay, El Pais. Chipukizi huyo mwenye miaka 19, alipata kura130 na kumwacha mshindi wa pili kwa kura 70 ambaye alikuwa mshambuliaji wa Chile, Eduardo Vargas aliyeisaidia klabu yake ya Universidad de Chile kutwaa kombe la Copa Sudamericana na taji la ligi ya ndani iliyotoa nafasi kwake kusajiliwa na Napoli. Mshiriki wa Neymar, katika timu ya Santos, Paulo Henrique Ganso alishika nafasi ya tatu, huku kocha wa Universidad de Chile, Jorge Sampaoli alikuwa kocha wa pili bora wa mwaka.