Neymar kuongoza kikosi cha Olimpiki

RIO DE JENEIRO, Brazil NEYMAR ataongoza kikosi cha Brazil kwenye mashindano ya soka ya Olimpiki jijini London. Pia katika kikosi hicho wameitwa Marcelo wa Real Madrid, Hulk wa Porto na Thiago Silva wa AC Milan. Hulk, Thiago na Marcelo wameitwa kama wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 23. Wachezaji watatu tu wenye umri zaidi ya miaka 23 ndio huruhusiwa kwenye vikosi vinavyoshiriki kwenye mashindano ya soka ya Olimpiki. Pamoja na kuwa na umri mdogo, Neymar tayari amekuwa anang'ara na kikosi cha wakubwa cha Brazil kwa muda mrefu sasa. Yosso wa AC Milan, Alexandre Pato naye atakuwemo kitakachoshiriki michuano hiyo. Brazil imepangwa katika Kundi la C ikiwa na timu za Misri, Belarus na New Zealand. Kikosi kamili kiko hivi Makipa:Rafael Cabral (Santos), Neto (Fiorentina) Mabeki: Marcelo (Real Madrid), Rafael (Manchester United), Danilo (Porto), Alex Sandro (Porto), Thiago Silva (AC Milan) Juan (Inter) na Bruno Uvini (Sao Paulo). Wachezaji wa kiungo ni Romulo (Vasco da Gama)Ganso (Santos), Oscar (Internacional), Sandro (Tottenham) na Lucas (Sao Paulo). Washambuliaji wanaounda kikosi hicho ni Neymar (Santos), Alexandre Pato (AC Milan), Leandro Damiao (Internacional) na Hulk (Porto).