Neymar 'apeta' kikosi cha Brazil Kombe la Dunia
Muktasari:
- Baada ya kusubiri kwa hamu, ulimwengu mzima wa soka umethibitishiwa kurejea kwa fundi huyo kwenye kikosi cha Brazil, baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Carlo Ancelotti amemtaja Neymar kwenye kikosi cha wachezaji 26 watakaoiwakilisha Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.
Baada ya kusubiri kwa hamu, ulimwengu mzima wa soka umethibitishiwa kurejea kwa fundi huyo kwenye kikosi cha Brazil, baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.
Kikosi cha Brazil kilichotajwa na kocha Carlo Ancelotti:
Makipa Alisson, Ederson, na Weverton.
Mabeki: Alex Sandro, Bremer, Danilo, Douglas Santos, Gabriel Magalhães, Ibañez, Léo Pereira, Marquinhos, na Wesley.
Viungo: Bruno Guimarães, Casemiro, Danilo S., Fabinho, pamoja na Lucas Paquetá.
Washambuliaji: Neymar Jr., Endrick, Gabriel Martinelli, Igor Thiago, Luiz Henrique, Matheus Cunha, Raphinha, Rayan, na Vini Jr.