Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Newcastle yamtenga Isak

Muktasari:

  • Hatma ya Isak Newcastle imekuwa ya kutatanisha tangu aliposhindwa kuungana na wachezaji wenzake katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya barani Asia, hali iliyotokana na Liverpool kuwa katika mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo, 25.

NEWCASTLE, ENGLAND: STRAIKA wa Newcastle na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak amewekwa kando na kikosi cha kwanza na kuamriwa afanye mazoezi peke yake, pia akiondolewa katila hafla maalum ya familia iliyoandaliwa na klabu kwa ajili ya wachezaji na wapendwa wao.

Hatma ya Isak Newcastle imekuwa ya kutatanisha tangu aliposhindwa kuungana na wachezaji wenzake katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya barani Asia, hali iliyotokana na Liverpool kuwa katika mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo, 25.

Taarifa zinasema tayari Liverpool iliwasilisha ofa, lakini ikakataliwa na Newcastle wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Sky Sports, Isak amekuwa akifanya mazoezi binafsi nchini Hispania, akitumia vifaa vya klabu yake ya zamani, Real Sociedad jambo linalodaiwa kufanyika kinyume na matakwa ya Newcastle United.

Awali, Isak alitarajiwa kurejea kwenye kituo cha mazoezi cha Newcastle Jumatano ya wiki iliyopita, lakini baadae akaambiwa anatakiwa kuripoti baada ya kumalizika kwa tukio la chakula cha pamoja na familia za wachezaji.

Hii ina maana Isak atakosa hafla hiyo ya kijamii, ambayo imekuwa sehemu ya kujenga mshikamano wa timu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England.

Wachezaji wenzake wa Newcastle walirejea England Jumatatu na kuanza mazoezi Jumatano baada ya kupumzika kwa siku moja. Hata hivyo, Isak bado hajaungana nao rasmi na ripoti zinadai ameambiwa asijiunge na vigogo wa timu hiyo.

Licha ya hali hiyo, kwa mujibu wa Chronicle Live, Isak anatarajiwa kucheza wikiendi hii kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Espanyol na Atletico Madrid, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya msimu mpya.

Taarifa nyingine zimefichua staa huyu alifanya baadhi ya makosa ambayo yamechangia kutojumuishwa katika kikosi kwenye baadhi ya shughuli muhimu.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe, alisema: "Hii ni Newcastle United. Mchezaji anawajibika kuwa sehemu ya timu na sehemu ya kikosi, hatutakubali mchezaji yeyote ambaye anatenda visivyo kuendelea kujumuika na wachezaji wengine kana kwamba ni kawaida."