Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

New Trafford... Bosi afichua shida ilipo

BOSI Pict

Muktasari:

  • Man United ilitambulisha mpango wake wa kujenga uwanja mapema Machi mwaka huu, sambamba na kubomoa Old Trafford ili kujenga uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 100,000 wanaoketi.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inafikiria mambo mawili katika vita yao ya kupata kipande cha ardhi kinachodaiwa ndicho kinachochelewesha kuanza kwa ujenzi wa uwanja mpya wa Pauni 2 bilioni.

Man United ilitambulisha mpango wake wa kujenga uwanja mapema Machi mwaka huu, sambamba na kubomoa Old Trafford ili kujenga uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 100,000 wanaoketi.

Mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Sir Jim Ratcliffe amekuwa na matumaini makubwa kwenye ujenzi wa uwanja huo uliopachikwa jina la ‘Wembley ya Kaskazini’, utakaokamilika 2030, lakini sasa shughuli ipo kwenye kununua kipande cha ardhi kinachodaiwa kumilikiwa na kampuni ya Freightliner.

Kwa mujibu wa Daily Mail, thamani ya kipande hicho cha ardhi ni Pauni 40 milioni, hivyo wanadhani Freightliner wanajaribu kupandisha thamani yake, kutokana na kutaka Pauni 400 milioni.

Kutokana na hilo, Man United inafikiria kutafuta suluhu ya kumaliza tatizo ili ipate ardhi hiyo na kuanza ujenzi.

Imeelezwa amri ya ulazima wa kuuzwa inaweza kutumika ili ardhi hiyo ipatikane, huku Man United ikipanga kuendeleza maeneo yanayozunguka uwanja.

Na ripoti hiyo inafichua Man United inaweza kununua kipende kidogo tu cha kujenga uwanja kisha eneo jingine italichukua baadaye.

Mradi huo wa ujenzi mpya wa uwanja unatarajia kutengeneza ajira mpya 92,000 na nyumba za makazi mapya zaidi ya 17,000, wakati huo huo ikidaiwa itavutia watalii zaidi ya 1.8 milioni.

Kwenye eneo la pembeni la uwanja huo mpya, kutajengwa makazi mapya ya kuvutia, maeneo ya starehe ili kulifanya eneo hilo liwe la kitalii, kuvutia watu wengi kuliko wanaokuja tu kwa ajili ya mechi za soka.