Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

New Caledonia, Jamaica kuamua DR Congo kushiriki Kombe la Dunia 2026

DR CONGO Pict

Muktasari:

  • Timu hizo sita zimepangwa kulingana na viwango vyao vya ubora kwenye chati za Fifa, ambapo timu mbili za juu, DR Congo inayoshika nafasi ya 56 na Iraq (58), zimekwenda moja kwa moja kwenye fainali za mchujo huo, huku Jamaica (70), Bolivia (76), Suriname (123) na New Caledonia (149) zinaanzia nusu fainali.

DR Congo itasubiri mshindi kati ya New Caledonia na Jamaica ili kucheza nayo katika mechi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 kupitia mchujo wa mabara (inter-confederation play-offs).

Mechi hizo zilizopangwa kuchezwa Machi 2026, DR Congo inasaka nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya mataifa tisa ya Afrika kufuzu moja kwa moja kupitia hatua ya makundi. Mataifa hayo ni Algeria, Cape Verde, Misri, Ghana, Ivory Coast, Morocco, Senegal, Afrika Kusini na Tunisia. Hivyo, DR Congo inaweza kuongeza idadi ya timu za Afrika kwenye fainali hizo kufikia 10 endapo itashinda mechi hiyo kwenye mchujo.

Mchujo huo wenye timu sita, mechi zimepangwa kuchezwa huko Mexico, moja ya nchi wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazoanza Juni 11, 2026 hadi Julai 19, 2026 zikishirikisha mataifa 48. Wenyeji wengine ni Canada na Marekani.

Katika droo iliyochezeshwa mchana wa leo Novemba 20, 2025 na kiungo wa zamani wa Ufaransa, Christian Karembeu, mchujo mwingine utazihusu Bolivia dhidi ya Suriname. Mshindi wa mechi hii anakwenda kucheza dhidi ya Iraq, kusaka atakayefuzu michuano hiyo.

Timu hizo sita zimepangwa kulingana na viwango vyao vya ubora kwenye chati za Fifa, ambapo timu mbili za juu, DR Congo inayoshika nafasi ya 56 na Iraq (58), zimekwenda moja kwa moja kwenye fainali za mchujo huo, huku Jamaica (70), Bolivia (76), Suriname (123) na New Caledonia (149) zinaanzia nusu fainali.