Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndoo ya UEFA 2024/25 inatua England

Ndoo Pict
Ndoo Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa mfumo mpya wa mashindano hayo, kuna mechi nane katika hatua ya ligi kabla ya raundi za mtoano. Timu nane bora zinapita kwenda hatua ya 16 bora kama mbegu, huku timu zinazoshika nafasi ya tisa hadi 24 zikicheza mechi ya mtoano ili kupata nane nyingine zitakazoungana na zile nane za kwanza kucheza 16 bora.

LONDON, ENGLAND: KOMPYUTA ambayo imekuwa ikitumika kutabiri ushindi na mabingwa wa ligi mbalimbali (Supercomputer) imeonyesha kuwa timu zitakazocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu zote zinatokea England.

Kwa mujibu wa mfumo mpya wa mashindano hayo, kuna mechi nane katika hatua ya ligi kabla ya raundi za mtoano. Timu nane bora zinapita kwenda hatua ya 16 bora kama mbegu, huku timu zinazoshika nafasi ya tisa hadi 24 zikicheza mechi ya mtoano ili kupata nane nyingine zitakazoungana na zile nane za kwanza kucheza 16 bora.

Hata hivyo, utabiri huo wa kompyuta unaonyesha Manchester City, Arsenal, Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid zote zitashiriki raundi ya mtoano pamoja na Aston Villa na Celtic. Vilevile Sporting Lisbon na Inter Milan zitaingia mtoano. Liverpool itamaliza hatua ya ligi ikiwa ya kwanza bila ya kupoteza mchezo ambapo itashinda mechi saba na sare moja. Vilevile PSG imetabiriwa kuangukia pua kwani itamaliza nafasi ya 27 katika msimamo. Imeonyeshwa pia katika mtoano Arsenal itakutana na Bayern Munich ambapo itashinda mabao 5-3, Liverpool itashinda dhidi ya Barcelona 2-1 katika matokeo ya jumla huku Man City ikiilaza Monaco 6-1.

Katika robo fainali Arsenal itaichapa Atalanta na Man City itatolewa na Real Madrid huku Liverpool ikiifuamua Sporting.

Nusu fainali Liverpool itaiondoa Real Madrid katika kwa mabao 4-2 na Arsenal itaichapa Inter Milan 4-3.

Kompyuta hiyo imetabiri kwamba Liverpool na Arsenal zitarudia rekodi ya 2021 ambapo ilikuwa mara ya mwisho kwa timu mbili kutoka nchi hiyo kucheza pamoja katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Manchester City iliilazwa na Chelsea kwa bao 1-0.

Na katika fainali hiyo, Supercomputer inaonyesha kwamba Liverpool itachukua kombe baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal.