Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balaa la Ulaya... Kuna mtu anapigwa

ITALIA Pict

Muktasari:

  • Kwenye mechi za kwanza, Inter ilifungana 3-3 na Barcelona, wakati PSG yenyewe ilitoka uwanjani Emirates kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao, Arsenal. Jambo hilo linafanya mechi za marudiano kutarajia kuwa na upinzani mkali.

MILAN, ITALIA: NI leo kama sio kesho. Ni kuhusu vipute vya marudiano vya hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo usiku wa Jumanne, Inter Milan itajimwaga kwenye uwanja wa nyumbani kukipiga na Barcelona, kabla ya usiku wa Jumanne, Paris Saint-Germain kuwa na shughuli pevu huko Parc des Princes mbele ya Arsenal.

Kwenye mechi za kwanza, Inter ilifungana 3-3 na Barcelona, wakati PSG yenyewe ilitoka uwanjani Emirates kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao, Arsenal. Jambo hilo linafanya mechi za marudiano kutarajia kuwa na upinzani mkali.

Miaka 19 imepita tangu Arsenal ilipofika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kupoteza mbele ya Barcelona katika mchezo uliogawanyika huko Paris, Ufaransa na itakwenda kwenye mechi ya nusu fainali ikijaribu kukwepa machungu hayo, itakapokipiga na PSG katika mechi ambayo, ukipigwa unatupwa nje.

PSG itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na faida ya kuongoza 1-0, shukrani kwa bao pekee la kumfukuzia Ballon d'Or, Ousmane Dembele alilofunga kwenye mechi ya kwanza, hivyo Arsenal itahitaji kupindua meza ili kufika fainali ya mwaka huu.

Arsenal iliitupa nje Real Madrid kwenye hatua ya robo fainali na kuona kama kazi ya mbele ingekuwa rahisi zaidi kabla ya kukutana na kigingi hicho kutoka kwa vijana wa Luis Enrique, ambao waliisukuma nje Liverpool kwenye hatua hiyo ya nane bora.

Hata hivyo, kuna timu mbili tu zilizotinga hatua inayofuata baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilipocheza nyumbani, hiyo ilikuwa Ajax dhidi ya Panathinaikos mwaka 1996 na mahasimu wa Arsenal, Tottenham Hotspur kwenye mechi dhidi ya Ajax tena mwaka 2019. Je, Arsenal itaingia kwenye orodha hiyo Jumatano?

Goncalo Ramos anaweza kuanza kwenye mechi hiyo, wakati kiungo wa Kikorea Lee Kang-in akiwa na hatihati kubwa baada ya kuwa majeruhi, lakini kwenye sehemu ya kiungo Vitinha na Fabian Ruiz wataungana na Joao Neves. Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia watakuwa kwenye safu ya ushambuliaji, huku Arsenal yenyewe ikimkaribisha kikosini Thomas Partey, ambaye alikosa mechi ya kwanza.

Partey na Declan Rice wataanza sambamba na nahodha Martin Odegaard, ikiwa ni injini muhimu kwenye kuhakikisha kikosi hicho cha Arsenal kinafanya mapinduzi kwenye mchezo huo wa ugenini

Vikosi vinavyotarajiwa;

PSG: Donnarumma; Hakimi, Marquinhos, Pacho, Mendes; Ruiz, Vitinha, Neves; Doue, Ramos, Kvaratskhelia

Arsenal: Raya; Timber, Saliba, Kiwior, Lewis-Skelly; Odegaard, Partey, Rice; Saka, Merino, Martinelli

Hata hivyo, mchakamchaka huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utaanza usiku wa leo Jumanne na Inter itakuwa na kazi moja ya kuhakikisha wanafanya kweli dhidi ya Barcelona baada ya kuwabana vyema kwenye mechi ya kwanza na kumalizika 3-3.

Mechi ya kwanza iliyofanyika Hispania ilishuhudia mabao sita, hivyo mashabiki wa soka wanasubiri kuona kile kitakachokwenda kutokea San Siro na Inter itahitaji kutinga fainali ili ikapambane kunasa taji la nne, huku Barca yenyewe ikifukuzia taji la sita.

Kwenye mchezo wa kwanza Marcus Thuram na Denzel Dumfries walifanya vizuri kwa upande wa Inter, lakini Barca ilijibu vyema mapigo kwa makali ya Lamine Yamal na Raphinha. Nani atatoboa?

Inter itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kuwahi kuitoa Barca kwenye mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010, wakati kikosi hicho kilipokuwa chini ya Kocha Jose Mourinho. Na sasa jukumu hilo lipo kwa Inzaghi.

Vikosi vitarajiwa;

Inter Milan: Sommer; Bisseck, Acerbi, Bastoni; Dumfries, Barella, Calhanoglu, Mkhitaryan, Dimarco; Arnautovic, Thuram

Barcelona: Szczesny; Garcia, Araujo, Cubarsi, Martinez; De Jong, Pedri; Yamal, Olmo, Raphinha; Torres