Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rodrygo achomoza usajili mpya Arsenal

TETESI Pict

Muktasari:

  • Rodrygo, 24, ambaye pia anaripotiwa kuzivutia Liverpool na Manchester United, amekuwa katika kiwango bora kutokana na kuitumikia Real Madrid kwa zaidi ya miaka sita sasa tangu 2019 na hajawahi kukosekana kabisa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

ARSENAL inakuwa ni timu ya hivi karibuni kuulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo Silva de Goes ‘Rodrygo’ ili kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Rodrygo, 24, ambaye pia anaripotiwa kuzivutia Liverpool na Manchester United, amekuwa katika kiwango bora kutokana na kuitumikia Real Madrid kwa zaidi ya miaka sita sasa tangu 2019 na hajawahi kukosekana kabisa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mchezaji huyo amekuwa akiwindwa na timu mbalimbali Ulaya kutokana ubora ambao amekuwa akiuonyesha Real Madrid, huku uwepo wa mastaa kama Kylian Mbappe na Vinicius JR ukidaiwa kumfanya aanze kufikiria kuondoka jijini Madrid.

Nyota huyo ambaye kabla ya kutua Real Madrid aliwahi kukipiga Santos ya kwao Brazil, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo Juni 30, 2018, ambapo msimu huu ameshafunga mabao sita na asisti sita katika mechi 30 za La Liga.


Desire Doue

REAL Madrid inadaiwa kujiweka mguu sawa kusaka saini ya mshambuliaji wa PSG na Ufaransa, Desire Doue, 19, kama chaguo la kwanza iwapo Rodrygo ataondoka kikosini dirisha lijalo la usajili la majira ya kiagazi. Doue iwapo ataondoka PSG, anatarajiwa kugharimu zaidi ya Pauni 85milioni, jambo linaweza kuwa gumu kwa timu za kawaida kumudu gharama yake, hivyo Madrid kubaki peke yake. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika Juni 30, 2029.


Morgan Gibbs-White

MANCHESTER City imeongeza juhudi katika harakati za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White kama mrithi wa muda mrefu wa Kevin De Bruyne. Inaelezwa Morgan mwenyewe ameonyesha kuvutiwa na ofa ya kutua katika kikosi hicho ambacho msimu huu akijawa na kiwango bora hasa kutokana na nyota wengi kukumbwa na majeraha. Mkataba wake unamalizika Juni 30, 2027.


James Maddison

KOCHA Pep Guardiola anamfikiria kiungo wa Totenham Hotspur, James Maddison, 28, ili akaimarishe eneo la kiungo la Manchester City msimu ujao analoamini huenda likayumba kutokana na viungo shoka, Kevin De Bruyne na Ilkay Gundogan kuondoka kikosini. Inadaiwa Man City ipo tayari kutumia Pauni 55.4m ili kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa England dirisha lijalo na atabakiza misimu mitatu kumaliza mkataba wake.


Casemiro

CASEMIRO yupo mbioni kupata nyongeza kubwa ya mshahara endapo Manchester United itatwaa taji la Europa League na hivyo kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ambapo pia huenda akaongeza mkataba mpya badala ya kumalizika 2026, ukamalizika 2027. Nyota  huyo,33, amekuwa wa moto katika mechi za karibuni za Ligi Kuu England na Europa, jambo ambalo linaushawishi uongozi kumuongezea mkataba mpya.


Ronald Araujo

INAELEZWA juhudi za Manchester United kumsajili beki wa kati wa Barcelona, Ronald Araujo, 26, zitapata nguvu zaidi endapo timu hiyo itashiriki  mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msim ujao. Araujo amekuwa hapati nafasi mara kwa mara katika kikosi hicho na sasa anashawishika kutaka kuondoka Barcelona kwenda kusaka maisha sehemu nyingine. Mkataba wake unamalizika 2031.


Bryan Mbeumo

CHELSEA iko tayari kuwasilisha ofa ya Pauni 51.1milioni kwa ajili ya mshambuliaji wa Brentford, Bryan Mbeumo, 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Manchester United, Arsenal, Liverpool na Newcastle United zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Cameroon. Mkataba wake unamalizika Juni, mwakani.


Joan Garcia

BOURNEMOUTH imejiingiza kwenye mbio za kumsajili kipa anayetakiwa na timu nyingi Ulaya, Joan Garcia, 24, wa Espanyol. Arsenal, Manchester United na Barcelona zote zinahusishwa kuwa na nia kubwa ya kumsajili kipa  huyo ambaye huenda akagharimu Pauni 25.5milioni. Mkataba wake unamalizika Juni 30, 2028.