Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Napoli kuwabania vigogo England kwa McTominay

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Hatua hiyo inakuja wakati ambao baadhi ya klabu za Ligi Kuu England ikiwemo Manchester United, Chelsea na Aston Villa zinaonyesha nia ya kumsajili kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

NAPOLI inadaiwa kuanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo kimataifa wa Scotland, Scott McTominay, 29.

Hatua hiyo inakuja wakati ambao baadhi ya klabu za Ligi Kuu England ikiwemo Manchester United, Chelsea na Aston Villa zinaonyesha nia ya kumsajili kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hali hiyo inaifanya Napoli kutaka kumpa mkataba mpya wa muda mrefu ambao utaiweka katika nafasi ya kupata pesa nyingi zaidi hata kama itaamua kumuuza. McTominay amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Napoli, na uongozi wa klabu hiyo unaamini kumbakiza staa huyo ni muhimu katika mipango ya ushindani wa misimu ujao.

Taarifa zinadai timu yake ya zamani, Man United, ambayo inatafuta mbadala wa Casemiro aliyetangazwa kuondoka mwisho wa msimu, inaamini staa huyo viatu hivyo vinamtosha.

Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajiwa kumalizika 2028. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 34.


Micky van de Ven

BARCELONA imeanza mazungumzo na wawakilishi wa beki wa Tottenham Hotspur, Micky van de Ven, 24, na inatarajiwa kutuma ofa ya kumsajili mwisho wa msimu.

Taarifa zinaeleza Barca inamchukulia beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi kama chaguo sahihi la kuimarisha safu ya ulinzi kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu. Hata hivyo, dili hilo halitakuwa rahisi kwani Spurs inathamini mchango wake.


Kevin Schade

WINGA wa Brentford, Kevin Schade, 24, ameendelea kuwa katika rada za timu mbalimbali Ulaya zinazotaka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Kwa mujibu wa taarifa, Schade anawindwa  na Tottenham Hotspur, Bayern Munich na Inter Milan ambazo zimeshaanza kuzungumza na wawakilishi wake. Mkataba wa sasa wa Schade unatarajiwa kumalizika 2028.


Andre Onana

MABOSI wa Trabzonspor ya Uturuki wameiambia Manchester United kwamba hawapo tayari kutoa Pauni 40 milioni kwa ajili ya kumnunua kipa wa kimataifa wa Cameroon, Andre Onana ambaye msimu huu anacheza katika kikosi vicho kwa mkopo.

Inaelezwa Onana mwenye umri wa miaka 29, anatamani kubaki Trabzonspor lakini changamoto kubwa inaonekana kuwa ni kiasi cha pesa kinachohitajika ili kufanikisha suala hilo.


Mason Mount

KIUNGO wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Mason Mount, 27, anadaiwa kuwa hana mpango wa kuondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya taarifa kudai kwamba anaweza kusepa kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza.

Inaelezwa Mount anataka kubaki na kupambania namba kwani anaamini suala la kucheza na kuwa tegemeo kwa Mashetani Wekundu linawezekana. Mkataba unamalizika 2028.


Phil Foden

MANCHESTER City inapanga kumpa kiungo wake wa kimataifa wa England, Phil Foden, mkataba mpya mara tu ule wa sasa utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Hata hivyo, mazungumzo yanatarajiwa kuwa magumu kutokana na kiwango cha hivi karibuni cha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kuonekana kushuka. Hata hivyo, inaelezwa Man City bado inaamini Foden ni muhimu kikosini.


William Osula

STRAIKA wa Newcastle United, William Osula amesisitiza kuwa hajui msimu ujao atacheza wapi au itakuwaje, lakini kwa sasa anapambana kuhakikisha anaitumikia Newcastle.

Hivi karibuni, Osula alidaiwa kuwa katika mpango wa kuondoka mwisho wa msimu kwa sababu mabosi wa timu hiyo hawaridhishwi na kiwango chake.

Mkataba wa staa huyo mwenye umri wa miaka 22 unatarajiwa kumalizika 2029 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 24.


Antoine Griezmann

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 34, ameamua kutoondoka Atletico Madrid katikati ya msimu huu licha ya kuwepo kwa ofa kutoka Orlando City.

Taarifa zinaeleza Orlando City ilionyesha nia ya kumsajili, lakini Griezmann alitaka kubaki Atletico walau hadi mwisho wa msimu.

Uamuzi huo aliuchukua akiamini halikuwa jambo la busara kuondoka wakati ambao timu ilikuwa inamhitaji.