Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Darwin Nunez anukia Chelsea, Newcastle pia ipo

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa mbali ya Chelsea, Newcastle United pia inahitaji huduma ya staa huyo ambaye amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Al-Hilal jambo linayomfanya kutaka kurudi Ulaya.

CHELSEA imeingia katika vita ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Al-Hilal ya Saudi Arabia na timu ya taifa ya Uruguay, Darwin Nunez, 26, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa mbali ya Chelsea, Newcastle United pia inahitaji huduma ya staa huyo ambaye amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Al-Hilal jambo linayomfanya kutaka kurudi Ulaya.

Kwa sasa kwa asilimia kubwa Al-Hilal imekuwa ikimtumia Karim Benzema, 38, aliyesajiliwa dirisha la majira ya baridi mwaka huu. Tangu kuanza kwa msimu huu, Nunez ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2028 amecheza mechi 24 za michuano yote, akifunga mabao tisa na kutoa asisti tano.

Staa huyo kwa sasa anapata mshahara unaofikia Pauni 400,000 kwa wiki lakini atahitajika kukubali kuupunguza ikiwa atataka kurudi Ulaya kwani hakuna timu inayoonekana kuwa tayari kumlipa kiasi hicho cha pesa kama mshahara. Inaelezwa ikiwa Chelsea itafanikiwa kumsajili kuna uwezekano mkubwa straika Leam Delap akaruhusiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.


Tino Livramento

MANCHESTER City wako tayari kuingia katika rekodi ya dunia ya ada ya usajili wa beki kwa kulipa Pauni 70 milioni ili kumsajili beki wa kulia wa kimataifa wa England, Tino Livramento, 23, kutoka Newcastle United dirisha lijalo la kiangazi. Man City wanaona Livramento ni chaguo muhimu kuimarisha safu ya ulinzi kutokana na umri wake na kiwango anachoonyesha kwa sasa. Iwapo dili hilo litakamilika litamweka Livramento kuwa mmoja wa mabeki ghali duniani.


Nico Schlotterbeck

BEKI wa kati wa kimataifa wa Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26, ambaye ana mkataba na Borussia Dortmund unaomalizika 2027, tayari ameanza kuingia kwenye rada za vigogo wa Ulaya. Miongoni mwa klabu zinazomfuatilia ni Real Madrid ambayo inamtaja kuwa mmoja wa mastaa walio katika orodha ya kuwasajili mwisho wa msimu, lakini pia Liverpool inamtamani. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote.


Santiago Gimenez

SUNDERLAND na West Ham United zimejitokeza kuonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Mexico, Santiago Gimenez, 24, dirisha lijalo la kiangazi. Taarifa zinaeleza Milan iko tayari kusikiliza ofa kutoka timu zinazomtaka nyota huyo ingawa itamuuza ikiwa tu itawasilishwa ofa nono mezani. Tangu kuanza kwa msimu huu, Gimenez amecheza mechi 11 michuano yote na kufunga bao moja. na amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha ya mara kwa mara.


Altay Bayindir

KIPA wa Manchester United, Altay Bayindir, 27, anatarajiwa kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu, huku klabu ya Uturuki, Besiktas, ikitajwa kuwa miongoni mwa timu anazoweza kutua. Taarifa zinaeleza Bayindir anatafuta nafasi ya kucheza mara kwa mara, jambo ambalo limekuwa gumu kulipata akiwa Manchester United. Mazungumzo ya awali yanatarajiwa kuanza kufanyika dirisha la majira ya kiangazi litakapofunguliwa.


Marcus Rashford

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya taifa ya England ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Barcelona, Marcus Rashford, 28, amekubali kupunguziwa mshahara pamoja na kuachana na baadhi ya bonasi ili kufanikisha dili la mkopo kutoka Manchester United kwenda Barcelona kubadilishwa kuwa la kudumu. Hatua hiyo imeonyesha dhamira ya Rashford kutaka kuendelea na maisha ya Camp Nou.


Dean Henderson

CRYSTAL Palace imeweka msimamo kuzuia ofa itakayowasilishwa kwa ajili ya kipa Dean Henderson, 28, anayewaniwa na Tottenham Hotspur na klabu nyingine za England. Henderson amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya Palace jambo linalosababisha mabosi kutokuwa na mpango wala mawazo ya kutaka kumuuza kwani wanafahamu itachukua muda kidogo kupata mbadala bora.


Teun Koopmeiners

JUVENTUS ipo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Teun Koopmeiners, 28, lakini inahitaji walau Euro 30 milioni ili kumuuza staa huyo. Koopmeiners anahusishwa na uhamisho kwenda Galatasaray na AS Roma, huku klabu hizo zikifuatilia kwa karibu hali yake. Hata hivyo, Juventus haitaruhusu mchezaji huyo kuondoka kirahisi bila ofa itakayokidhi bei rasmi waliyoiweka kumuuza nyota huyo.