Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nainggolan amshambulia Scott McTominay, amuita mchezaji wa kawaida Italia

Muktasari:


  • McTominay ambaye alihamia Napoli 2024 kwa ada ya pauni 25.7 milioni, amekuwa mmoja muhimu timu hiyo. Katika kipindi cha misimu miwili, kiungo huyo tayari amefunga mabao 26 na hata kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa Msimu katika Serie A baada ya kuiongoza Napoli kutwaa ubingwa.

NAPLES, ITALIA: KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Scott McTominay amezua mjadala nchini Italia ambako amekosolewa na staa wa zamani wa Serie A, Radja Nainggolan akimtaja Mwingereza huyo kuwa mchezaji wa kawaida.

McTominay ambaye alihamia Napoli 2024 kwa ada ya pauni 25.7 milioni, amekuwa mmoja muhimu timu hiyo. Katika kipindi cha misimu miwili, kiungo huyo tayari amefunga mabao 26 na hata kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa Msimu katika Serie A baada ya kuiongoza Napoli kutwaa ubingwa.

Hata hivyo, mafanikio hayo hayajamvutia Nainggolan ambaye aliwahi kung’ara katika klabu za AS Roma na Inter Milan. Akizungumza katika kipindi cha Sky Calcio, Mbelgiji huyo hakuficha hisia zake.

“Simpendi. Anafunga mabao mengi lakini kwenye uchezaji wa jumla hana ubora wa kucheza kati ya mistari. Ni mchezaji wa kawaida,” alisema.

Kauli hiyo imekuja licha ya ukweli kwamba McTominay ameendelea kusifiwa na wachambuzi wengi kutokana na mchango wake mkubwa Napoli, hasa uwezo wake wa kufunga na kuiongoza timu.

Hii sio mara ya kwanza kwa Nainggolan kutoa kauli tata. Kiungo huyo ambaye sasa anacheza soka la daraja la chini nchini Ubelgiji pia alijilinganisha na baadhi ya mastaa wakubwa wa dunia, akidai kuwa katika ubora wake aliwazidi ikiwemo McTominay na Hakan Calhanoglu.

Hata hivyo, alikiri kuwa wachezaji kama Kevin De Bruyne na Luka Modric wako juu zaidi huku akimtaja Nicolo Barella kuwa bora zaidi kwake kutokana na mchango wake mkubwa uwanjani hata kama hafungi mabao mengi.

Mbali na hilo, Nainggolan aliwahi pia kuikosoa kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji kilichokuwa na mastaa kama Romelu Lukaku, Eden Hazard, De Bruyne na Thibaut Courtois, akidai kilikuwa na mastaa wengi wenye ubinafsi jambo lililochangia kushindwa kufikia mafanikio makubwa kimataifa.