Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mziki wa Palmer hapo Manchester United

PALMER Pict

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni kiungo wa Chelsea, Cole Palmer, yuko tayari kurejea katika mji wake wa utotoni baada ya miaka miwili na nusu akiwa mbali.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United kwenye kikosi chao tayari ina mmoja wa viungo bora kabisa wa kushambulia duniani, lakini bado inataka kuongeza mwingine.

Kinachoelezwa ni kiungo wa Chelsea, Cole Palmer, yuko tayari kurejea katika mji wake wa utotoni baada ya miaka miwili na nusu akiwa mbali.

Palmer, 23, alihamia Chelsea kutoka Manchester City mwaka 2023 na amekuwa nyota matata kabisa huko Stamford Bridge.

Hata hivyo, inaaminika Palmer hajisikii kutulia kabisa jijini London na angepokea kwa mikono miwili ofa kutoka Man United. Palmer alikulia Wythenshawe na alikuwa akiishabikia Man United tangu utotoni, hivyo hurudi Manchester mara kwa mara. Lakini, hataki kurudi Man City kwa uhamisho wowote, jambo linaloacha wazi chaguo moja tu la kwenda Man United endapo kama anataka kurudi jijini Manchester.

Kwa Man United, ambao wamekuwa wakihusishwa na Palmer kwa muda mrefu tangu alipoanza kung’ara chini ya Mauricio Pochettino na baadaye Enzo Maresca, hili linaweza kuwa tukio la ndoto kwao endapo watainasa saini yake. Man United inamtazama Palmer kama mtu sahihi wa kuja kuvaa buti za Bruno Fernandes endapo ataondoka, lakini itakuwa furaha kubwa kwao kama Mreno huyo atabaki ili wawili hao wacheze pamoja Old Trafford.

Palmer ni habari nyingine, akiwa amefunga mabao 48 katika mechi 108 alizocheza Chelsea huku akiwa asisti mara 28. Mabao 41 ni ya Ligi Kuu England.

Palmer alionekana kupungua kiwango msimu uliopita na amekuwa akisumbuliwa na majeraha tangu alipocheza Kombe la Dunia la Klabu majira ya joto, lakini bado ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa zaidi. Iwapo Man United itamsajili, ataongeza ubora mkubwa kikosini, lakini ataingiaje kwenye kikosi?

Hivi hapa namna tatu ambazo Palmer anaweza kuchezeshwa katika kikosi cha Man United.

PAL 02
  1. Palmer kama No.10

Iwapo Bruno ataondoka na Man United ina makubaliano nahodha wao anaweza kuondoka kwa Pauni 57 milioni, basi Palmer atakuwa mbadala wa moja kwa moja. Bruno ana miezi 18 iliyobaki kwenye mkataba wake, lakini Man United ina chaguo la kumwongezea mwaka zaidi kama itaamua kubaki naye ili kuwafanya kuwa na fowadi yenye makali ya kutisha na kwenye dirisha lililopita iliwaongeza pia Matheus Cunha, Benjamin Sesko na Bryan Mbeumo.

Akiongezeka Palmer na kama Bruno ataendelea kubaki, basi Sesko itamlazimu kuanzia benchini.

Bila shaka Man United itaingia sokoni kusaka kiungo wa kati kuchukua nafasi ya Casemiro, anayeoondoka mwisho wa msimu. Carlos Baleba anapewa nafasi kubwa ya kunaswa licha ya viungo wengine kama Adam Wharton na Elliot Anderson nao wakipigiwa hesabu. Kama Bruno ataondoka na Palmer akinaswa, basi atakwenda kucheza kwenye nafasi yake anayoipenda, Namba 10 kwenye fomesheni ya 4-2-3-1.

Palmer acheze kwenye kikosi chenye Amad, Mbeumo, Cunha na Sesko bila shaka itakuwa timu itakayofunga mabao mengi sana.

Kikosi: Lammens; Dalot, Yoro, Martinez, Dorgu; Mainoo, Baleba; Amad, Palmer, Mbeumo; Sesko.

PAL 03

2. Palmer kama winga wa kulia

Lakini je, Bruno ataendelea kubaki na Palmer acheze pamoja naye? Hilo ni wazo la ndoto kwa wapenda ubunifu na mipira ya mbali. Palmer alitoa kiwango chake bora alipocheza winga wa kulia chini ya Pochettino huko Chelsea, akikatiza ndani na kuleta madhara makubwa.

Akiwa na Diogo Dalot pembeni kumpa upana na Fernandes katikati, kuna uwezekano mkubwa wa ushirikiano mzuri. Hapa, Man United itapata ubora wa Palmer na Fernandes kwa pamoja, huku Mbeumo akiwa kushoto japokuwa nafasi hiyo pia inaweza kuchukuliwa na Amad au hata Cunha, ikiwa Dorgu atapanda kushambulia. Makocha wengi hupenda kujaza maeneo matano ya ushambuliaji uwanjani na kikosi hiki kina machaguo tele. Mbeumo au Cunha wanaweza hata kucheza kama mshambuliaji wa uongo (false nine).

Kikosi: Lammens; Dalot, Yoro, Martinez, Dorgu; Mainoo, Baleba; Palmer, Fernandes, Mbeumo; Sesko.

PAL 01

3. Staili inayoitwa Mti wa Krismasi

Huu ni mfumo mwembamba wa 4-2-3-1 unaowakusanya karibu washambuliaji wote wa Man United. Palmer angekuwa upande wa kulia kati ya viungo watatu wa kushambulia (No.10s). Mfumo huu wa Mti wa Krismasi unafaa pasi za haraka na ubunifu wa papo kwa papo kati ya wachezaji wenye nguvu.

Kuna uwezekano mkubwa wa wachezaji kubadilishana nafasi na kuzurura ili kuwasambaratisha wapinzani. Palmer pia amewahi kucheza kama kiungo wa kulia (No.8) Chelsea, akibadilika kuwa No.10. Fernandes alichezeshwa nyuma kidogo chini ya Ruben Amorim na kama Man United watataka kuimarisha kiungo katika mfumo wa 4-3-3, wanaweza kufanya hivyo kwa kuwa Palmer na Cunha pia wanaweza kushuka chini kusaidia.

Kikosi: Lammens; Dalot, Yoro, Martinez, Dorgu; Mainoo, Baleba; Palmer, Cunha, Fernandes; Mbeumo.