Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cole Palmer ampa hofu gwiji wa Chelsea

PALMER Pict

Muktasari:

  • Palmer amekuwa usajili bora zaidi chini ya umiliki wa bilionea Todd Boehly, kipindi ambacho kimeshuhudia wachezaji wengi wa gharama kubwa wakishindwa kuonyesha kiwango walichotarajiwa.

LONDON, ENGLAND: ALIYEKUWA beki kisiki wa Chelsea, Marcel Desailly anaamini kiungo Cole Palmer anaweza kuwasilisha ombi la kuondoka endapo hataona dalili yoyote ya kwamba timu hiyo inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England ndani ya miaka miwili ijayo.

Palmer amekuwa usajili bora zaidi chini ya umiliki wa bilionea Todd Boehly, kipindi ambacho kimeshuhudia wachezaji wengi wa gharama kubwa wakishindwa kuonyesha kiwango walichotarajiwa.

Uhamisho wake wa Pauni 40 milioni kutoka Manchester City umeonekana kuwa biashara nzuri sana na ameendelea kung’ara tangu alipoanza kupewa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza Stamford Bridge.

Hata hivyo, Chelsea kwa sasa haipo kwenye mbio za ubingwa, huku lengo lao likiwa ni kumaliza ndani ya nafasi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amepona maumivu ya kinena na kurejea katika nafasi yake ya kawaida, lakini Desailly ana hofu anaweza kutamani kujiunga na klabu itakayojenga mfumo wa mchezo unaomzunguka yeye.

Kumekuwa na mazungumzo yasiyoepukika kuhusu kurejea Etihad, huku Manchester United klabu aliyokuwa akiishabikia Palmer akiwa mdogo ikitajwa pia kama uwezekano wa yeye kutua, jambo ambalo Desailly halioni kuwa la kushangaza.

Akizungumza na Card Player, Desailly amesema: “Swali ni kama anahisi Chelsea wataweza kushinda Ligi Kuu katika misimu miwili ijayo. Kama hahisi hivyo, nina uhakika ataomba kuhamia klabu itakayojenga mfumo wa mchezo unaomzunguka yeye.”

Nahodha huyo wa zamani wa Chelsea aliongeza: “Kama Cole Palmer ataamua kuondoka Chelsea, hilo ni uamuzi wake, lakini ninachotaka aheshimu klabu, kwa sababu wao ndio waliompa zana za kumfanya awe mchezaji alipo sasa. Ningependa sana abaki Stamford Bridge kwa sababu ana jukumu muhimu sana katika timu, hata kama Enzo Maresca amekuwa akimtumia katika nafasi mbalimbali.

"Ninaamini Palmer anahitaji uthabiti zaidi na mfumo ulioundwa kwa ajili yake, lakini bado anapaswa kupona kabisa jeraha la kinena na kurejea katika kiwango chake kamili. Kiwango chake cha hivi karibuni kinajieleza chenyewe, hivyo anapaswa kubaki mnyenyekevu na kurudi kusaidia timu, bila kujali kama ataondoka au atabaki.”

Palmer alifunga mabao 25 katika msimu wake wa kwanza huko Stamford Bridge na ametoa mchango mkubwa pia katika timu ya taifa ya England.

Chelsea sasa ina kocha mpya, Liam Rosenior na athari yake, pamoja na jinsi atakavyomtumia Palmer, inaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kuamua mustakabali wa klabu na mchezaji huyo mbunifu ndani ya uwanja.