Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzigo wa England unapigwa tena!

EPL Pict

Muktasari:

  • Huko Emirates, Jumapili kutakuwa na balaa zito, wakati Arsenal itakapokipiga na Chelsea, mechi itakayohusisha vita mbili, ile ya kusaka ubingwa na nyingine ya kufukuzia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: SHUGHULI ni pevu. Ndicho unachoweza kusema kufuatia mchakamchaka wa mechi za Ligi Kuu England zitakazopigwa wikiendi hii.

Huko Emirates, Jumapili kutakuwa na balaa zito, wakati Arsenal itakapokipiga na Chelsea, mechi itakayohusisha vita mbili, ile ya kusaka ubingwa na nyingine ya kufukuzia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Arsenal ipo kwenye mbio za ubingwa, hivyo itahitaji ushindi kwenye mechi hiyo ya dabi ya London ili kuendelea kutanua pengo la pointi kwenye kilele cha msimamo wa ligi, lakini Chelsea nayo ikihitaji ushindi ili kuhakikisha inaendelea kubaki ndani ya Top Four. Patamu hapo.

Arsenal imeweka pengo la pointi tano dhidi ya Manchester City kwenye nafasi ya pili, lakini pengo hilo linaweza kupungua hadi pointi mbili, endapo kama kikosi cha Pep Guardiola kitaibuka na ushindi kitakapokwenda kucheza ugenini dhidi ya Leeds United, Jumamosi.

Ushindi kwa Man City utamfanya Mikel Arteta na chama lake la Arsenal kuwa kwenye presha kubwa ya kuhakikisha inaichapa Chelsea ili kulinda pengo la pointi tano, la mambo yanaweza kuwa magumu kwenye mbio hizo za ubingwa.

Mechi nyingine za Jumamosi, Bournemouth itakipiga na Sunderland, Burnley na Brentford, Newcastle United na Everton, wakati Liverpool itaendelea na kampeni ya kuhakikisha haing'oki nje ya eneo lenye tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kukipiga na West Ham.

Kwa upande za mechi Jumapili, ukiweka kando kipute cha Arsenal na Chelsea, vita nyingine ya Top Four itawahusu Manchester United watakaokuwa uwanjani Old Trafford kukipiga na Crystal Palace, huku Fulham ikiwa na kasheshe la kukutana na wababe wenzao wa London, Tottenham Hotspur wakati Brighton itakuwa nyumbani kuonyeshana ubabe na Nottingham Forest.