Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yapata pigo kisa kiungo

Muktasari:

  • Staa huyo wa kimataifa wa Japan, alitolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kwanza kwake kwenye EPL tangu kuanza kwa msimu huu.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imepata pigo kubwa baada ya kumpoteza kiungo wao Wataru Endo kutokana na jeraha kubwa alilopata katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Sunderland wiki iliyopita.

Staa huyo wa kimataifa wa Japan, alitolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kwanza kwake kwenye EPL tangu kuanza kwa msimu huu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alichaguliwa kucheza kama beki wa kulia, huku kocha Arne Slot akikosa chaguonyingine, kwani mabeki wa kulia wa asili Conor Bradley na Jeremie Frimpong nao walikuwa majeruhi.

Endo amecheza mechi 12 tu katika mashindano yote kwa Liverpool msimu huu kutokana na ushindani mkali wa nafasi. Hata hivyo, nahodha wa Liverpool Virgil van Dijk alisema mbali ya kukosa huduma ya Endo kiwanjani pia wanaumizwa na kumkosa kwenye chumba cha kubadilishia nguo kutokana na ucheshi wake na mchango wake linapokuja suala la kuwaweka sawa kisaikolojia.

“Ni jambo la kusikitisha, sote tuliumia sana baada ya mechi ya Sunderland,” alisema Van Dijk. “Niliwahi kupata jeraha kama hilo nilipokuwa Southampton, jeraha la mguu, na si rahisi kulikabili.

Lakini tupo hapa kwa ajili yake, tutakuwa pamoja naye kila hatua na kumpa msaada wote anaohitaji. Siyo hali nzuri, yeye ni mchezaji muhimu sana na anayeheshimika ndani ya timu, ni mmoja wa viongozi na daima huongoza kwa vitendo.

“Uwanjani anajitoa kwa asilimia mia moja. Ni pigo kubwa lakini tunapaswa kulikubali na tutafanya hivyo. Tunatumaini haitamchukua muda mrefu sana kurudi, lakini inaonekana itachukua muda."

Kocha wa Liverpool, Arne Slot bado hajasema kuhusu muda ambao Endo atautumia kuuguza jeraha lake na baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brighton kwenye Kombe la FA mwishoni mwa wiki, alisema:

“Kuna uwezekano Endo akarejea kabla ya msimu kuisha, lakini atakuwa nje kwa muda. Hatuwezi kusema ni muda gani hasa kwa sasa. Kila jeraha linakuwa tofauti. Wakati mwingine unaweza kufanya uchunguzi mara moja, wakati mwingine unahitaji siku chache kuona undani wa tatizo."

“Hatakuwa kwenye kikosi wiki ijayo, wala hatakuwa kwenye kikosi mwezi ujao. Lakini tunatumaini mwishoni mwa msimu anaweza kupata nafasi ya kuwa nasi tena."