Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZIGO HUO! Chukua hizi tano za Arsenal ikiichapa Madrid

MZIGO Pict

Muktasari:

  • Kiungo Mikel Merino ndiye aliyefunga bao la tatu dakika 15 kabla ya filimbi ya mwisho ya mchezo na kuiweka Real Madrid, ambao ni mabingwa watetezi, kwenye mlima mrefu wa kutinga raundi inayofuata.

LONDON, ENGLAND: MABAO mawili ya friikiki matata kabisa yaliyofungwa na Declan Rice yameiweka mahali pazuri Arsenal kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwachapa Real Madrid 3-0 uwanjani Emirates.

Kiungo Mikel Merino ndiye aliyefunga bao la tatu dakika 15 kabla ya filimbi ya mwisho ya mchezo na kuiweka Real Madrid, ambao ni mabingwa watetezi, kwenye mlima mrefu wa kutinga raundi inayofuata.

Rice alifunga bao la kwanza kwa staili kali sana alipopiga friikiki ya mita 30, ambapo mpira ulionekana kama unatoka nje kabla ya kukunja na kuingia nyavuni kipa Thibaut Courtois akiwa hana la kufanya. Arsenal haikusubiri muda mrefu kufunga bao la pili, Rice tena alimteka kipa Courtois kwa friikiki nyingine matata kabisa.

Kama bao la kwanza lilikuwa zuri, bali la pili ni tamu zaidi. Mpigo wake ulikuwa matata, ulionyesha mpira unakoelekea.

Merino, ambaye aligomewa mara mbili wakati ubao ukisomeka 1-0, baada ya David Alaba kuokoa kwenye mstari shuti lake, alifunga bao kwa umaliziani bora kabisa na kumteka kipa Courtois. Arsenal 3-0.

Arsenal itakwenda Bernabeu wiki ijayo katika mechi muhimu ya kutinga nusu fainali, huku wenyeji wao Los Blancos hawatakuwa na huduma ya Eduardo Camavinga kwenye mechi hiyo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu Emirates.

Mechi hiyo ya Emirates imeacha vifungashio vitano kwa mashabiki kwenda navyo kujadiliana navyo kwao.

MZ 01

1. Arsenal ni wafalme mpya wa mipira iliyokufa

Real Madrid ilipata shida sana kuzuia mipira iliyokufa ya Arsenal. Mara zote Arsenal iliposogea kwenye goli la Real Madrid kupiga mipira hiyo, mambo yaliyoenekana kuwa na presha kubwa kwa vijana wa Carlo Ancelotti. Na kuthibitisha hilo, hata mabao matatu waliyoruhusu kwenye nyavu zao, miwili ilitokana na mipira iliyokufa, friikiki za Rice.

MZ 02

2. Courtois bado kipa wa viwango

Kipa Thibaut Courtois anafahamu eneo lake la kutamba na kuonyesha kiwango bora ni kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Amefanya maajabu mengi kwenye michuano hiyo na hata kwenye mechi hiyo ya Emirates, ubora wake uliifanya Real Madrid isipoteze kwa mabao mengi zaidi ya hayo waliyofungwa. Bila shaka kipa huyo ni silaha ya Real Madrid kwenye michuano mikubwa, huku akijipa lawama mwenyewe kwa friikiki za Arsenal zilizotinga nyavuni mwake.

MZ 03

3. Saka kama hajatoka kuumwa

Mwanzoni Saka alionekana kama mambo hayapo vizuri, lakini baadaye alibadilika na kuonyesha kile anachoweza kukifanya kwa uwezo mkubwa. Winga huyo alichofanya uwanjani kwenye mechi hiyo utadhani hakuwa ametokea kwenye maumivu yaliyomfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kuugusa majeraha ya kufanyiwa upasuaji. Hata faulo iliyosababisha bao la kwanza ilisababishwa na winga huyo, ambaye muda wote alikuwa tishio hadi alipotoka uwanjani.

MZ 04

4. Kazi na umri ni vitu vinavyoendana

Wakati Myles Lewis-Skelly wa Arsenal anazaliwa, Luka Modric alikuwa tayari amecheza mechi 10 kwenye kikosi cha Croatia na kufunga bao moja. Hilo linaweza kukuonyesha vizazi tofauti vilivyokutana kwenye mechi hiyo ya Emirates, ambapo kuna mtu alikuwa anaelekea nyakati za mwisho za soka lake na hakika ni hivyo baada ya Modric kushindwa kuonyesha kiwango bora uwanjani, huku Lewis-Skelly muda wote alionekana kuwa bora uwanjani.

MZ 05

5. Real Madrid ina kazi nzito

Miaka sita iliyopita, Liverpool iliingia uwanjani kwenye mechi ya marudiano ya hatua ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa na kazi moja ya kupindua matokeo ya mabao matatu. Real Madrid inafahamu wazi hilo limeshawahi kufanyika huko nyuma, lakini ukweli inahitaji kucheza kwa kiwango bora sana kwenye mechi hiyo ya marudiano. Bado mapema kuwasema Real Madrid kwamba wameshakufa kwenye michuano hii ya Ulaya, lakini ukweli utabaki palepale wana kazi nzito na wenyewe wanalitambua hilo.


TAKWIMU ZA MECHI YENYEWE

Mashuti golini: Arsenal 11, Madrid 3

Mashuti yote: Arsenal 12, Madrid 9

Mashuti kuzuiwa: Arsenal 1, Madrid 2

Umiliki mpira: Arsenal 54%, Madrid 46%

Pasi zote: Arsenal 490, Madrid 435

Pasi sahihi: Arsenal 438, Madrid 376

Kucheza faulo: Arsenal 8, Madrid 9

Kupiga takolin: Arsenal 12, Madrid 15

Kupiga kona: Arsenal 5, Madrid 3