Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamba ulioanguka ukibeba historia ya soka Afrika

ISSA HAYATOU

Muktasari:

  • Hayatou ambaye anashikilia rekodi ya kuhudumu kiti hicho kikubwa kwenye soka la Afrika kwa muda mrefu (miaka 28), alifariki dunia Ufaransa alikokua akiishi.

RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Issa Hayatou alifariki dunia juzi Alhamisi ikiwa ni saa 24 kabla ya kutimiza umri wa miaka 78.

Hayatou ambaye anashikilia rekodi ya kuhudumu kiti hicho kikubwa kwenye soka la Afrika kwa muda mrefu (miaka 28), alifariki dunia Ufaransa alikokua akiishi.

Tangu mwaka 1988 hadi 2017 ndipo alipoachia kiti hicho, huku pia akisimama kama rais wa muda wa Shirikisho la Soka duniani kuanzia mwaka 2015 hadi 2016 na alishikilia nafasi hiyo baada ya Sepp Blatter kusimamishwa kutokana na tuhuma.

Moja kati ya stori za kukumbukwa ilikuwa ni usaliti aliofanyiwa na marais wa vyama vya soka Afrika katika uchaguzi wa urais wa FIFA mwaka 2002 alipokuwa akichuana na Blatter.

Kabla ya yote, awali katika miaka ya 90, timu nyingi za Afrika zilikuwa zikiachia wachezaji wao kwenda Ulaya na Hayatou aliona hali hiyo inachangia udumavu wa soka la Afrika kwani wengi walipokuwa wakifika Ulaya walikuwa wakibadilishwa uraia na kuzitumikia nchi hizo hali inayozidhoofisha timu za taifa lilipokuwa suala la michuano ya Kombe la Dunia au Olimpiki.

Hayatou hakupenda kuona wachezaji wa Kiafrika wanaenda nje na alikuwa akisema huo ni kama ukoloni kwani nchi za Ulaya zilikuwa zikichukua wachezaji wao wenye vipaji bora kisha wanaleta makocha wao wa kawaida.

Hata hivyo, juhudi zake hazikuzaa matunda kwani timu nyingi ziliendelea na utaratibu huo wa kuuza wachezaji wao kwenda barani humo.

Miaka kadhaa baadae Hayatou alifanya mazungumzo na Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) na kuanzisha mahusiano ambayo yalikuwa makubwa kiasi cha kumsapoti katika uchaguzi wa mwaka 2002 na alipata kura  56 ambazo nyingi zilitoka barani Ulaya.

Hata hivyo, licha ya kuwa rais wa CAF, nchi nyingi za Afrika ziliungana kumpigia kura mpinzani wake Blatter kwenye uchaguzi huo uliofanyika Korea Kusini na hadi leo imebaki kuwa moja ya kumbukumbu mbaya katika histori ya Hayatou.

Mzee huyu ambaye alianza harakati zake kama mwalimu wa somo la Fizikia ni kaka wa aliyekuwa waziri mkuu wa Cameroon Sadou Hayatou.

Alianzia harakati zake kama mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya taifa ya Cameroon kabla ya kuingia katika soka mwaka 1974 akiwa na umri wa miaka 28 alipochaguliwa kuwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Cameroon.

Baada ya kuwa katibu mkuu kwa muda, mwaka 1986 alichaguliwa kuwa rais wa shirisho hilo huku taarifa zikidai alikuwa na ushawishi mkubwa kutokana na cheo cha kaka yake ambaye mbali ya kuwa waziri mkuu alikuwa ofisa na mtu wa karibu wa rais wa Cameroon, Paul Biya.

Licha ya ukubwa na cheo ambacho kaka yake na familia yake kwa jumla walikuwa navyo, Hayatou anakumbukwa kwa kuwa mtu wa kuthubutu katika kila jambo.

Katika kipindi chake alifanikiwa kuisaidia Afrika kuongeza idadi ya timu katika ushiriki wa Kombe la Dunia kutoka mbili hadi tano.

Pia aliisaidia Afrika Kusini kupata uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na alishiriki kuanzia mchakato wa kuwasilisha maombi hadi kupewa dhamana hiyo.

Mwaka huo ulikuwa ni wa mafanikio kwa Hayatou kwani aliiwezesha Afrika kuingiza timu sita kwa mara ya kwanza.

Kwenye uongozi wake alibadilisha Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa upande wa idadi ya timu shiriki kutoka nane hadi 16, kisha akafanya maboresho ya michuano mbalimbali kwa ngazi ya klabu ili kuongeza ushiriki wa timu nyingi zaidi ikiwa pamoja na kuanzia michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2004.

Hadi anastaafu mambo ya soka alikuwa ni Mwenyekiti wa bodi ya Akademi ya Soka Cameroon.

Mwaka 2010, aliripotiwa kupokea rushwa ya Dola 10,000 katika miaka ya 90 kutoka kwa kampuni iitwayo ISL ili kuwapa haki ya matangazo ya televisheni.

Hayatou alipinga tuhuma hizo na kusema pesa ziliingia katika akaunti ya CAF na sio yake, baada ya taarifa hiyo kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ikasema itachunguza kwa sababu alikuwa mwanachama wao.

Hakuishia hapo, mwaka 2011 jarida la The Sunday Times, iliripotiwa Hayatou aliyekuwa anashikilia cheo cha mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA, pamoja na mjumbe mwenzake  Jacques Anouma kutoka Ivory Coast walipokea rushwa ya Dola 1.5 milioni kutoka Qatar ili wasaidie kushawishi nchi hiyo kupata uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022.

Hadi umauti unamkuta Hayatou alikuwa kwenye ndoa na kupata watoto wanne.