Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu hapa msimamo kuhusu straika Gyokeres

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Na rais wa klabu hiyo ya Ureno, Frederico Varandas amewaonya Arsenal kwa kuiambia “lipeni pesa, kaeni pembeni.”

LISBON, URENO: SPORTING Lisbon imeambia Arsenal haiwezi kushusha kabisa bei inayomuuza straika wake wa mabao Viktor Gyokeres baada ya kusakwa sana kwenye dirisha hili la usajili.

Na rais wa klabu hiyo ya Ureno, Frederico Varandas amewaonya Arsenal kwa kuiambia “lipeni pesa, kaeni pembeni.”

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ameweka kipaumbele chake kwenye usajili wa dirisha hili kwamba anataka straika ili kuongeza nguvu kwenye safu hiyo, ambapo sambamba na Gyokeres, staa mwingine kwenye rada zake ni mkali wa Red Bull Leipzig, Benjamin Sesko.

Hata hivyo, dili zote hizo mbili bado zipo kwenye shaka kubwa.

Gyokeres, 27, alikasirishwa na mabosi wa Sporting kwa kudai kwamba wamekiuka makubaliano ambapo awali walidai watamruhusu kuondoka kwa Pauni 60 milioni -- lakini iliongeza na kudai inahitaji Pauni 80 milioni, ikiweka kipengele hicho kwenye mkataba wake.

Na kinachoelezwa straika huyo wa Sweden sasa amegoma kuendelea kuichezea Sporting.

Arteta alikuwa na matumaini ya kumnasa kwa pesa ndogo, lakini Varandas alisema atamuuza mchezaji huyo kwa kuzingatia thamani halisi ya soko lake.

Arsenal kwa sasa imehamishia nguvu zake kwenye usajili wa kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi na wapinzani wao kwenye mbio za kumsajili Gyokeres, Manchester United wao baada ya kumsajili Matheus Cunha kwa sasa wanapambania saini ya Bryan Mbeumo wa Brentford.

Varandas alitishia kumbakiza Gyokeres Ureno endapo kama Arsenal itaendelea kupeleka ofa ndogo, wakati matumaini yake walau kupata Pauni 70 milioni kwenye mauzo ya straika huyo.

Alisema: “Sporting imekuwa watulivu wakubwa juu ya ishu ya Viktor Gyokeres. Hatutaki kumuuza, lakini tunatambua ndoto za Viktor na wachezaji wengine wowote. Baada ya wiki kadhaa za vikao, hatujaandika kipengele chochote kwenye mkataba kuhusu bei ya Viktor. Mchezaji anajua, wakala wanajua na naweza kuwathibitishia, Viktor hawezi kuondoka kwa Pauni 60 milioni.”

Man United nayo inafuatilia ishu ya Gyokeres na sasa itageukia kwa mchezaji huyo itakapokamilisha dili la kumchukua Mbeumo.