Msikie Conte kuhusu Kane

LONDON, ENGLAND. HARRY Kane amehusishwa kwenye tetesi za usajili dirisha la kiangazi na taarifa zimeripoti huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu huku Antonio Conte akikiri kuhusu hatima yake.

Hivi karibuni taarifa ziliripoti Tottenham Hotspurs itakubali kumuuza Kane kwa kitita cha Pauni 100 milioni, Manchester United ikihusishwa kwenye dili hilo kwasababu imeonyesha nia ya kumsajili.

Aidha kwa mujibu wa ripoti Spurs ipo tayari kutibua mpango huo ili Kane asiondoke licha ya mkataba wake unaelekea ukingoni, lakini Conte akadi hana uhakika kama atabaki.

"Bila shaka mabosi wanataka Kane aendelee kuichezea klabu yao kwa muda mrefu, unapokuwa na mchezaji bora kama Kane,bila shaka utataka aendelee kuwepo, lakini kwenye mpira lolote linaweza kutokea, huwezi kutabiri masuala kama haya, lakini nadhani haya sio maamuzi yangu, haya ni maamuzi ya klabu na mchezaji mwenyewe,"  alisema Kane

Kane ameendelea kukiwasha msimu huu,amefunga mabao 22 na kutengeneza asisti nne katika mashindano yote aliyocheza msimu huu akimfukuzia mkali wa mabao anayekipiga Manchester City, Erling Haaland.

Wiki kadhaa iliyopita nyota wa zamani aliyewahi kukipiga Spurs, Peter Crouch alikiri huenda Kane akaondoka kutokana na mwenendo mbovu wa timu msimu huu, kwasasa timu hiyo imeondolewa katika michuano yote msimu huu. Mkongwe huyo akasisitiza Kane anafukuzia mataji kwasababu kama rekodi ameshavunja sana ndani ya klabu hiyo.

Tottenham inapambana kwenye ligi ili ifuzu michuano Ligi Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kung'olewa dhidi ya AC Milan wiki iliyopita na kuhusu hatima ya Kane itafahamika mwisho wa msimu.

Taarifa ziliripoti Man United imeanza kumnyemelea straika huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye mkataba wake wa tamalizika itakapofika mwaka 2024.