Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshahara wa Sesko, Gyokeres wajadiliwa

MSHAHARA Pict

Muktasari:

  • Newcastle ilihitaji saini yake na kumpa ofa ya kumlipa mshahara mkubwa, lakini Sesko alivutiwa na mipango ya kocha Ruben Amorin na kuchagua Old Trafford.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA, Benjamin Sesko analipwa mshahara kiduchu kwenye Ligi Kuu England kuliko anavyolipwa mpachika mabao mwenzake mpya katika ligi hiyo, Viktor Gyokeres baada ya kugomea ofa za kwenda kujiunga na timu ambazo zingemlipa mkwanja mrefu na kuchagua kutua Manchester United.

Newcastle ilihitaji saini yake na kumpa ofa ya kumlipa mshahara mkubwa, lakini Sesko alivutiwa na mipango ya kocha Ruben Amorin na kuchagua Old Trafford.

Sesko amejiunga na Man United kwa mkataba wa miaka mitano kutoka RB Leipzig alikonaswa kwa Pauni 74 milioni, ambapo imetangulizwa kulipwa Pauni 66.4 milioni na nyongeza ya Pauni 7.6 milioni.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 22 analipwa mshahara wa Pauni 160,000 kwa wiki, ikiwa ni zaidi ya Pauni 8.3 milioni kwa mwaka. Jambo hilo linamfanya Sesko kuwa mbali sana na orodha ya mastaa wanaolipwa mshahara mkubwa huko Old Trafford, Casemiro akiongoza kwa kulipwa Pauni 350,000 kwa wiki, sawa na Pauni 18.2 milioni kwa mwaka.

Ni wazi, Sesko alikataa pesa nyingi kwenda kujiunga na kocha Amorim badala ya kwenda kwa Eddie Howe, ambako angevuna mkwanja mrefu.

Wakati huo, straika mwenzake mpya, Gyokeres, ambaye amejiunga na Arsenal akitokea Sporting Lisbon kwa dili la Pauni 64 milioni, anakwenda kulipwa mshahara mkubwa kwenye mkataba wake wa miaka mitano, ambapo analipwa Pauni 200,000 kwa wiki, sawa na Pauni 10.4 milioni kwa mwaka kabla ya malipo mengine ya bonasi. Ni Declan Rice, Martin Odegaard, Gabriel Jesus na Kai Havertz pekee ndio wanaolipwa mshahara mkubwa Emirates kumzidi Gyokeres.

Kwa maana hiyo, Sesko mshahara wake upo nyuma kwa Pauni 40,000 kwa wiki kwa kulinganisha kiasi anacholipwa Gyokeres.

Hata hivyo, endapo kama Man United itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi mshahara wa Sesko utapanda na kuwa Pauni 200,000 kwa wiki na kumfikia Gyokeres.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anaamini straika wake mpya atafunga mabao ya kutosha tu kutokana na ukali wake wa kutumia vyema nafasi za kufunga, huku Sesko akiipa Man United matumaini makubwa kwamba atakuwa suluhisho la mabao kwa kuwa atacheza na watengeneza nafasi wazuri, Cunha na Mbeumo.