Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho awapiga kijembe Chelsea

MOURINHO Pict

Muktasari:

  • Chelsea ilikuwa timu ya kwanza kushinda taji la Kombe la Dunia la Klabu katika mtindo mpya, wakati ilipoichapa PSG mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.

LISBON, URENO: JOSE Mourinho ameipiga kijembe Chelsea kwamba kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu ni muhimu kwao, lakini upande wake alitazama michuano hiyo kama vile ambavyo mara zote amekuwa akienda Marekani kwenye pre-season.

Chelsea ilikuwa timu ya kwanza kushinda taji la Kombe la Dunia la Klabu katika mtindo mpya, wakati ilipoichapa PSG mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.

Lakini, kocha wa Chelsea, Enzo Maresca aliyapa umuhimu mkubwa mashindano hayo ya Kombe la Dunia la Klabu aliposema: “Nadhani yatakwenda kuwa muhimu kama Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo kushinda michuano hiyo ni kama kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.”

Hilo alisema licha ya timu wababe kama Barcelona na Liverpool kutokuwapo kwenye michuano hiyo. Na Mourinho, ambaye kwa sasa ni kocha wa Fenerbahce, alisema mashindano hayo yalikuwa madogo kuliko hata mechi za pre-season alizowahi kwenda kucheza kwenye ardhi hiyo ya Marekani.

Mourinho, ambaye alijipachika jina la Special One aliiambia Canal 11: "Hili Kombe la Dunia la Klabu lilionyesha kijana mdogo kuwa na msimu mzuri Chelsea, Cole Palmer. Lakini, zilipofika mechi za nusu fainali zilinikumbusha mimi nilivyokuwa nakwenda Marekani kwenye pre-season na timu zangu za Real Madrid na Inter, inanikumbusha mechi nilizocheza huko.

"Hivyo, nadhani taji la Kombe la Dunia la Klabu lilikuwa muhimu zaidi kwa Chelsea, kwa sababu watauza zaidi jezi na nembo yao. Nadhani, PSG walikuwa washindi wakubwa wa msimu huu, kwa sababu ya walichofanya kwenye ligi ya ndani, na pia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na namna walivyofanya ikiwa haina wachezaji wake wote mahiri."