Mourinho amtolea macho Sanchez

Muktasari:
- Hata hivyo, Mourinho tayari ameanza kujipanga kwa msimu ujao bada ya kuanza kufanya mawasiliano na Arsenal juu ya nia yake ya kumsajili Alex Sanchez ambaye yupo kwenye mipangoyake ya kumsajili kwenye kikosi cha Manchester United msimu ujao.
London, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameamua kujipanga kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake msimu ujao pamoja na kuhakikisha inashiriki mashindao ya Ligi ya Mabingwa mwakani.
Iwapo Manchester United itafanikiwa kufuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda kwenye Ligi ya Europa hiyo itakuwa nafasi yao nzuri zaidi.
Hata hivyo, Mourinho tayari ameanza kujipanga kwa msimu ujao bada ya kuanza kufanya mawasiliano na Arsenal juu ya nia yake ya kumsajili Alex Sanchez ambaye yupo kwenye mipangoyake ya kumsajili kwenye kikosi cha Manchester United msimu ujao.
Baada ya Mourinho kujitoa kwenye mbio za ubingwa, sasa ameonekana kujielekeza zaidi kwenye mipango ya kukiimarisha kikosi cha Man United kitakachosheheni vipaji kwa kuanza na kumnyakua mshambuliaji wa Arsenal, Sanchez.
Raia huyo wa Chile amekuwa akihusishwa muda mrefu kuhamia klabu za jijini Manchester ambapo anaonekana kuwa kwenye mpango wa kuodoka Emirates wakati wa msimu wa kiangazi.
Pia, Chelsea inahusishwa kutaka kumng’oa mchezaji huyo ambapo kocha Antonio Conte alijatwa wiki hii kuanza mchakato.
“Unajua sipendi kuzungumzia kuhusu wachezaji wa klabu nyingine siyo jambo la busara kuzungumzia klabu nyingine kwa sasa siyo muda mwafaka kuzungumzia jambo hili,” alisema Conte.