Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wa EPL: Arsenal yakaba kileleni, vita ya kushuka daraja yanoga

EPL Pict

Muktasari:

  • Manchester United na Liverpool wote walishinda ili kuimarisha nafasi zao katika tano bora, huku Aston Villa wakipunguzwa kasi kidogo, ingawa bado wanadhibiti hatima yao mbele ya wanaowafuatia. Upande wa chini wa msimamo, ushindi wa kwanza wa Tottenham Hotspur 2026 uliwapa morali mastaa, lakini bado wako katika eneo la kushuka daraja, huku West Ham United na Nottingham Forest pia wakipata ushindi muhimu.

NEWCASTLE, ENGLAND: VITA mbalimbali zinaendelea katika ligi tano bora za Ulaya kwa sasa, huku pendwa ya England ikipigwa tena leo baada ya Leeds United na Burnley kumalizana katika mzunguko wa 35, jana usiku.

Wakati Manchester City ikiwa kwenye michuano ya FA mwishoni mwa wiki iliyopita, Arsenal walitumia nafasi hiyo kurejea kileleni kwa ushindi mwembamba dhidi ya Newcastle United, ambao bado hawapo katika kiwango kizuri na wanashuka kwenye msimamo.

Manchester United na Liverpool wote walishinda ili kuimarisha nafasi zao katika tano bora, huku Aston Villa wakipunguzwa kasi kidogo, ingawa bado wanadhibiti hatima yao mbele ya wanaowafuatia. Upande wa chini wa msimamo, ushindi wa kwanza wa Tottenham Hotspur 2026 uliwapa morali mastaa, lakini bado wako katika eneo la kushuka daraja, huku West Ham United na Nottingham Forest pia wakipata ushindi muhimu.

Raundi ya 35 itashuhudia mechi zikichezwa leo Jumamosi, kesho na keshokutwa katika ratiba nyingine yenye michezo mingi ambayo inaweza kuwa na athari kubwa juu na chini ya msimamo.

EP 01

Leeds United wanaendelea kupigania kubaki katika ligi dhidi ya Burnley walioshuka daraja Ijumaa, huku West Ham wakitafuta kufanya vivyo hivyo watakaposafiri kwenda Brentford katika moja ya mechi tatu za leo Jumamosi inayoanza saa 9 alasiri. Arsenal wanaweza kuongeza pengo kileleni dhidi ya Fulham baadaye, huku Bournemouth wakitaka kuongeza rekodi bora ya kutopoteza mechi dhidi ya Crystal Palace, kesho Jumapili.

Mechi kubwa ya wikiendi itakuwa kati ya Manchester United na Liverpool, huku Jumatatu ikiwa na michezo miwili, ambapo Chelsea wanatafuta kurejea kwenye mstari dhidi ya Nottingham Forest kabla ya Manchester City kusafiri kwenda Everton.

EP 02

SIKIA HII

Kwa kuanzia, vinara wa ligi hiyo, Arsenal wanaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda wikiendi hii dhidi ya Fulham, nyumbani.

West Ham United waliowashinda Everton kwa mbinde mwishoni mwa wiki iliyopita hawawezi kumudu kupoteza pointi nyingi katika vita ya kushuka daraja, lakini wanakabiliwa na kazi ngumu dhidi ya Brentford wanaopigania nafasi ya kufuzu mashindano ya klabu Ulaya.

The Hammers, ambao wana tofauti ya pointi mbili juu ya mstari wa kushuka daraja wamepoteza mechi saba kati ya tisa dhidi ya Brentford wakishinda mara moja na sare moja. Hiki ndicho kiwango chao cha juu zaidi cha kupoteza dhidi ya timu yoyote waliyokutana nayo mara tano au zaidi (asilimia 78), huku pia wakifungwa katika mechi zote tisa dhidi ya Brentford katika mashindano hayo.

EP 03

Brentford hawajashinda katika mechi sita za mwisho za nyumbani (sare mara nne, kupoteza mbili), lakini kikosi cha West Ham United chini ya kocha Nuno Espirito Santo kinaweza kuwa na faraja kwamba Brentford wameshinda mechi mbili tu kati ya 15 za mwisho za ligi za timu za London (sare mara sita, kupoteza saba).

Nao Brighton wana nafasi ya kuimarisha nafasi ya sita dhidi ya Newcastle United wasio katika kiwango kizuri, na baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 Oktoba, mwaka jana wanatafuta kukamilisha mara ya pili kuwafunga Magpies katika msimu mmoja. Hata hivyo, mechi ngumu St. James’ Park anapewa nafasi kubwa ya kushinda huku Brighton ikiwa na kiwango kidogo ilhali pia sare ikiwa na uwezekano wa kutokea.

Brighton wameshinda mechi sita kati ya nane zilizopita (sare moja, kupoteza moja), idadi sawa na walivyoshinda katika mechi 23 zilizotangulia (sare tisa, kupoteza nane), ambapo wamefunga angalau mabao mawili katika kila moja ya mechi nne zilizopita. Newcastle, kwa upande mwingine, wamepoteza mechi 16 msimu huu zikiwemo nne za mwisho mfululizo, huku saba kati ya hizo zikiwa nyumbani. Pande zote mbili zinatafuta kumaliza mwenendo mbaya wakati Wolves waliokwishashuka daraja wanapokutana na Sunderland. Wolves walifungwa bao 1-0 na Tottenham Hotspur katika mechi ya mwisho, huku Sunderland wakipokea kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Nottingham Forest.

Hata hivyo, Wolves inapewa nafasi kubwa kushinda katika mechi ya leo dhidi ya Sunderland, huku sare ikiwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutokea na hii ni licha ya Sunderland kushinda mechi mbili za mwisho dhidi ya Wolves, waliopoteza mechi 23 msimu huu, sawa na rekodi yao mbaya zaidi katika msimu wa mechi 38, na wameshinda mechi moja kati ya 18 za mwisho za mwezi Mei (sare mara nne, kupoteza 13).

EP 04

Nayo Arsenal baada ya kurejea kileleni kwa ushindi dhidi ya Newcastle inaweza kuongeza tofauti hadi pointi sita dhidi ya Manchester City kwa ushindi dhidi ya Fulham. The Gunners waliotoa sare ya bao 1-1 na Atletico Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wana nafasi kubwa zaidi ya ushindi wikiendi hii.

Itakumbukwa kwamba Arsenal hawajawahi kupoteza katika mechi 32 za nyumbani dhidi ya Fulham (ushindi mara 25 na sare tisa), pia wamefungwa mabao 11 katika mechi 17 za nyumbani msimu huu na wameshindwa kufunga mara moja tu wakiwa katika Uwanja wa Emirates.

Hii siyo habari nzuri kwa Fulham ambao bado wana matumaini ya kumaliza katika nafasi za kufuzu Ulaya, kwani wameshinda mechi moja kati ya 15 dhidi ya Arsenal (sare nne, kupoteza 10). Fulham pia wameshindwa kufunga katika mechi nne kati ya sita zilizopita, ingawa walishinda zote mbili walizofunga.

Kesho Jumapili, Bournemouth wanatafuta kuongeza rekodi ya mechi 14 bila kupoteza dhidi ya Crystal Palace, huku wakiwa hatarini kupoteza nafasi ya mashindano ya klabu Ulaya, hivyo watapambana vilivyo wakiwa hawajapoteza katika mechi tano za mwisho dhidi ya Palace (ushindi mara mbili na sare tatu).

Lakini, Palace watatoa upinzani mkali; wamecheza bila kufungwa katika mechi tano kati ya nane za ugenini dhidi ya Bournemouth, lakini kwa ujumla katika mechi za karibuni ugenini wamepoteza mechi saba kati ya 13 za mwisho (ushindi mara tano, sare moja).

Hakuna timu yenye tofauti mbaya zaidi ya pointi zinazopatikana na kupotea kupitia mabao ya dakika ya 90 au zaidi kuliko Bournemouth (-3), huku Palace wakiwa bora zaidi (+6).

Nao Manchester United na Liverpool watakutana wakisaka kuimarisha nafasi zao katika tano bora, ambapo United wako nafasi ya tatu wakiwa juu kwa pointi tatu dhidi ya Liverpool, lakini wameshinda mechi tatu tu kati ya 19 dhidi ya Liverpool (sare tisa, wakipoteza saba). Hata hivyo, katika siku za karibuni wako vizuri na wanashinda bila tatizo lolote. Tangu kocha Michael Carrick aichukue timu hiyo, United wamekusanya pointi nyingi kuliko timu yoyote (29).

Kwa upande wa Liverpool wameshinda mechi tatu kati ya tano za ugenini dhidi ya United, sawa na walivyofanya katika mechi 18 zilizotangulia. Hivyo inaonekana kuwapo sare yenye uwezekano mkubwa zaidi. Liverpool wanaweza kumkosa Mohamed Salah kutokana na jeraha, na hiyo itamaanisha atakosa nafasi ya mwisho ya kucheza dhidi ya United akiwa amefunga mabao mengi zaidi ya ugenini dhidi yao (saba) kuliko mchezaji yeyote.

Mchezo mwingine utawashuhudia Tottenham Hotspur walioshinda mechi yao ya kwanza mwaka huu dhidi ya Wolves, lakini bado wako kwenye hatari ya kushuka na wakikutana na Aston Villa. Spurs wako nyuma kwa pointi mbili kutoka eneo salama, na wana nafasi ya ndogo ya kushinda dhidi ya Villa, ingawa hawajawahi kuwafunga Spurs nyumbani mfululizo tangu 2004. Hakuna mechi 21 zilizopita kati ya Villa na Spurs iliyomalizika kwa sare hivyo lolote linaweza kutokea.