Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mostafa Shobeir; Mtoto wa elfu 2 aliyeanza mbele ya mkongwe El-Shenawy

Muktasari:

  • Shobeir aliyezaliwa Mei 5, 2000 ambapo sasa ana umri wa miaka 26, ni mzaliwa wa jijini Giza nchini Misri huku akiwa anacheza klabu ya Al Ahly na mkongwe Mohamed El-Shenawy ambaye leo amekaa benchi akimshuhudia bwana mdogo huyo akipeperusha bendera ya taifa lao.

MISRI imeanza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa kumtumia Mostafa Shobeir kama kipa namba moja.

Shobeir aliyezaliwa Mei 5, 2000 ambapo sasa ana umri wa miaka 26, ni mzaliwa wa jijini Giza nchini Misri huku akiwa anacheza klabu ya Al Ahly na mkongwe Mohamed El-Shenawy ambaye leo amekaa benchi akimshuhudia bwana mdogo huyo akipeperusha bendera ya taifa lao.

Kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2026, Shobeir alikuwa ameichezea timu ya taifa ya Misri mechi nane ikiwamo moja dhidi ya Brazil katika kichapo cha 2-1, Juni 7, 2026, huku pia akiidakia Al Ahly mara 20 katika mashindano tofauti msimu wa 2025-2026.

Haikuwa jambo la uhakika kwamba angechaguliwa kipa huyo mbele ya El Shenawy mwenye umri wa miaka 37, lakini jina la Shobeir ambaye mkataba wake na Al Ahly unamalizika Juni 30, 2026 ndilo lililoonekana kwenye kikosi cha kwanza.

Kipa huyo anayekuja kwa kasi, ameshindwa kuondoka na clean sheet dhidi ya safu ya ushambuliaji yenye vipaji ya Ubelgiji akiruhusu bao moja wakati timu hizo zikitoka sare ya 1-1 katika mechi ya kundi G.

Shobeir aliyefanya sevu tatu kwa muda wote wa dakika tisini dhidi ya Ubelgiji, ni kipa wa kizazi cha pili nchini Misri.

Baba yake, Ahmed Shobeir, pia alikuwa kipa wa timu ya taifa ya Misri maarufu kama Mafarao.

Baadaye Ahmed alikuja kuwa makamu wa rais wa Chama cha Soka Misri (EFA).

Katika maisha yake ya uchezaji, Ahmed aliichezea Al Ahly kwa kipindi chote cha taaluma yake na aliichezea Misri mara 107.

Ahmed pia alihusika katika sare ya mabao 0-0 dhidi ya Ireland kwenye Kombe lq Dunia 1990, mechi ambayo ilizua mjadala mkubwa.

Wakati huo sheria ya kurudisha mpira kwa kipa (back-pass rule) ilikuwa bado haijaanzishwa. Hali hiyo iliifanya Misri kuendelea kumrudishia mpira Ahmed mara kwa mara, jambo lililosababisha mchezo huo kukosolewa na wengi kwa kuwa wa kuchosha na usiovutia.