Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndiye Vozinha kipa wa Cape Verde aliyeiduwaza Hispania

Muktasari:

  • Vozinho, mwenye umri wa miaka 40, alizaliwa Juni 3, 1986 katika mji wa Mindelo nchini Cape Verde na kwa zaidi ya muongo mmoja amekuwa chaguo la kwanza langoni mwa taifa hilo la visiwa vya Afrika Magharibi.

KIPA mkongwe wa timu ya taifa ya Cape Verde, Josimar José Évora Dias maarufu kama Vozinha, ameonyesha ubora wa juu akifanya 'sevu' nne kipindi cha kwanza dhidi ya Hispania katika mechi ya Kombe la Dunia 2026.

Vozinho, mwenye umri wa miaka 40, alizaliwa Juni 3, 1986 katika mji wa Mindelo nchini Cape Verde na kwa zaidi ya muongo mmoja amekuwa chaguo la kwanza langoni mwa taifa hilo la visiwa vya Afrika Magharibi.

Kipa huyo anayekipiga katika klabu ya GD Chaves nchini Ureno, alianza kuitumikia Cape Verde 2012 na hadi sasa amecheza zaidi ya mechi 80 za kimataifa, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika historia ya timu hiyo.

Umahiri wake ulionekana zaidi katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), ambapo ameshiriki matoleo kadhaa ikiwemo 2013, 2015, 2021 na 2023, akiisaidia Cape Verde kufikia mafanikio makubwa dhidi ya mataifa yenye nguvu barani Afrika.

Katika Kombe la Dunia 2026, Vozinho ameendelea kuvutia mashabiki wengi wa soka duniani kwa kuonyesha kiwango bora licha ya umri wake huku akiishangaza Hispania iliyoonekana ingeshinda mabao mengi.

Katika mechi dhidi ya Hispania inayoendelea hadi kufikia dakika ya 85 matokeo yakiwa 0-0, amefanya mfululizo uokoaji mabao takribani mara saba hali iliyoifanya Cape Verde kuendelea kupambana dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya.

Akizungumza na mitandao ya FIFA 2024, Vozinho alisema ndoto yake kubwa ni kuiona Cape Verde ikifanya makubwa katika soka la dunia na kuendelea kuhamasisha vijana wa taifa hilo kuamini kuwa hakuna lisilowezekana.

Kutokana na uzoefu, utulivu na uongozi wake uwanjani, Vozinho ameendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa makipa wengi wa Afrika na moja ya silaha muhimu zinazoiwezesha Cape Verde kushindana na mataifa makubwa katika soka la kimataifa.