Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mosquera amtia presha Arteta, majeruhi kibao

Muktasari:

  • Arsenal ilishuhudia vita yao ya kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu England zilikumbana na kigingi Jumamosi wakati ilipochapwa 2-1 na Aston Villa uwanjani Villa Park. Emi Buendia alifunga bao la ushindi dakika za majeruhi na kuwatibulia Arsenal.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amethibitisha beki Cristhian Mosquera anakabiliwa na wiki kadhaa za kukaa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu aliyopata kwenye mechi ya kipigo kutoka kwa Aston Villa.

Arsenal ilishuhudia vita yao ya kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu England zilikumbana na kigingi Jumamosi wakati ilipochapwa 2-1 na Aston Villa uwanjani Villa Park. Emi Buendia alifunga bao la ushindi dakika za majeruhi na kuwatibulia Arsenal.

Arsenal ilicheza mechi hiyo bila ya huduma ya mabeki wake wawili wa kati wale ambao wamekuwa wakianzishwa mara nyingi Gabriel Magalhaes na William Saliba kutokana na kuwa majeruhi, ambapo Jurrien Timber na Piero Hincapie walianzishwa.

Mosquera naye alikosekana kwenye kikosi kutokana na kupata maumivu ya enka aliyoyapata kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brentford katikati ya wiki.

Akizungumza baada ya kipigo cha Villa Park, kocha Arteta alisema beki huyo Mhispaniola atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, aliposema: "Atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa. Kwa bahati mbaya, imekuwa tofauti na tulivyotarajia, kwa namna tulivyokuwa tukimwangalia. Hivyo, atakuwa nje kwa wiki kadhaa."

Arsenal ilirejea kwenye njia zake za ushindi baada ya kuichapa Brentford baada ya kutokea kwenye sare ya 1-1 na Chelsea.

Ushindi dhidi ya Aston Villa ungewafanya kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane kabla ya Manchester City haijacheza.

Lakini, kipigo hicho na ushindi wa Man City wa mabao 3-0 dhidi ya Sunderland, umefanya pengo la pointi kwenye msimamo huo kuwa mbili, Arsenal ikiongoza.

Aston Villa ilitangulia kufunga bao kupitia kwa Matty Cash kabla ya Arsenal kuwazazisha kupitia kwa Leandro Trossard. Lakini, vijana wa Unai Emery walihakikisha pointi zote tatu zinabaki Villa Park baada ya Buendia kufunga bao la ushindi kwenye dakika za majeruhi kuipa Aston Villa ushindi muhimu na kuitibulia Arsenal mipango.