Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco yaiwekea ngumu Brazil Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Mara ya mwisho kwa Brazil kuanza kwa sare kwenye mechi yake ya kwanza kwenye Kombe la Dunia ilikuwa Juni 3,1978 ilipotoa sare kama hiyo dhidi ya Sweden, kwenye fainali zilizofanyika nchini Argentina.

Morocco imeanza Fainali za Kombe la Dunia kibabe baada ya kuikalia kooni Brazil,ikilazimisha sare ya bao 1-1.

Mara ya mwisho kwa Brazil kuanza kwa sare kwenye mechi yake ya kwanza kwenye Kombe la Dunia ilikuwa Juni 3,1978 ilipotoa sare kama hiyo dhidi ya Sweden, kwenye fainali zilizofanyika nchini Argentina.

Morocco imekuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 21 , kupitia Ismael Saibari akifunga bao safi la kiufundi, akipokea pasi ya kiungo wake Brahim Diaz.

Brazil maarufu kwa jina la Selecao, ikasawazisha bao hilo dakika ya  32 kupita s Vinicius Junior, akifunga bao zuri akitengenezewa pasi ya mwisho na Bruno Guimares.

Timu zote zimeonyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo huku makipa wakipa wakifanya kazi kubwa ya kuzima mashambulizi ambapo kipa wa  Morocco Yassine Bounou ameokoa mashamulizi manne huku mwenzake Allison Becker akifanya hivyo mara mbili.

Brazil imeonyesha kiwango kizuri ikitawala umiliki wa mpira kwenye vipindi vyote lakini ikakosa makali ya kutengeneza mashambulizi makali na kuweza kuyatumia.