Bao la Khoukhi dakika za mwisho laiokoa Qatar Kombe la Dunia
Muktasari:
- Bao la dakika 90+5 kwenye dakika sita za nyongeza likifungwa na beki wa kati Boualem Khoukhi kwa kichwa akipokea krosi ya Homam Al Amin limeipa Qatar pointi ya kwanza ya kihistoria kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Qatar imeukataa unyonge baada ya kugomea kipigo mbele ya Uswisi, ikisawazisha dakika za jioni mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Bao la dakika 90+5 kwenye dakika sita za nyongeza likifungwa na beki wa kati Boualem Khoukhi kwa kichwa akipokea krosi ya Homam Al Amin limeipa Qatar pointi ya kwanza ya kihistoria kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Uswisi ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake Breel Embolo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17 baada ya kiungo Remo Freuler kuchezewa vibaya na kipa wa QatarMahmoud Abunada.
Kipa huyo Abunada amekuwa na dakika 90 bora akifanya kazi kubwa kuzuia mashambulizi makali ya Uswisi ambayo yangekuwa mabao ya wazi.
Uswisi itajilaumu yenyewe kushindwa kutengeneza matokeo baada ya kutawala vizuri mchezo huo ikipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Matokeo hayo yanalifanya kundi B kuwa gumu ambapo kila mchezo umemalizika kwa sare na kuzifanya timu zote kuwa na pointi moja kila moja ambapo mapema Jana wenyeji wenza Canada ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bosnia- Herzegovina.
Kwenye mchezo huo mtoto wa staa wa zamani wa Simba Hassan Afif, Aqram Afif mwenyenasili ya Tanzania aliyechukua uraia wa Qatar, amecheza kwa dakika 90