Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco bado inautolea macho uenyeji Kombe la Dunia la Klabu 2029

MOROCCO Pict

Muktasari:

  • Michuano ya Kombe la Dunia la Klabu ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2025 nchini Marekani, ambapo Chelsea ilishinda taji dhidi ya Paris Saint-Germain katika fainali ya kwanza. Sasa, mashabiki na wadau wa soka wanazingatia michuano inayofuata mwaka 2029, ambapo mataifa kadhaa yanatarajiwa kuwasilisha zabuni ya kuwania kuwa mwenyeji.

NCHI ya Morocco bado ina dhamira ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu 2029 kwa kushirikiana na Hispania, ikiamini imekidhi vigezo vyote vya kupewa nafasi hiyo na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Michuano ya Kombe la Dunia la Klabu ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2025 nchini Marekani, ambapo Chelsea ilishinda taji dhidi ya Paris Saint-Germain katika fainali ya kwanza. Sasa, mashabiki na wadau wa soka wanazingatia michuano inayofuata mwaka 2029, ambapo mataifa kadhaa yanatarajiwa kuwasilisha zabuni ya kuwania kuwa mwenyeji.

Morocco imeoneysha kuwa na miundombinu madhubuti ya kuandaa michuano mikubwa, baada ya kuwa mwenyeji wa fainali za AFCON 2025 zilizofanyika kwa mafanikio makubwa, huku Senegal ikitawazwa kuwa bingwa baada ya kumfunga mwenyeji katika mechi ya fainali.

Hispania kwa upande wake tayari inajiandaa kuwa miongoni mwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2030 kwa kushirikiana na Ureno na Morocco, hivyo ushirikiano wa kuandaa Kombe la Dunia la Klabu 2029 kunachukuliwa kama sehemu ya kunogesha maandalizi ya makubwa ya soka duniani.

Michuano ya Kombe la Dunia la Klabu 2029, inatarajia kuongeza timu shiriki kutoka 32 hadi 48. Katika mfumo uliopendekezwa, Ulaya itapata nafasi 16 badala ya 12, ikiruhusu uwakilishi mpana na kufungua mlango kwa klabu kubwa zilizoshindwa kushiriki awali, ikiwemo Barcelona, Liverpool na Manchester United.

Kwa upande wa Afrika, bara hilo linaweza kuwakilishwa na klabu 6 hadi 7, jambo litakalotoa msukumo mkubwa kwa soka la klabu barani Afrika na kuongeza mwonekano wake katika kiwango cha kimataifa.

Mashindano haya yanatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa Bara la Afrika kuonesha uwezo wake katika kuandaa matukio makubwa ya soka duniani.