Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Monaco yapata tiba ya kona za Arsenal

Monaco Pict
Monaco Pict

Muktasari:

  • Monaco ilichapwa 3-0 kwenye mchezo huo, Bukayo Saka akifunga mara mbili na Kai Havertz moja. Ushindi huo umeifanya Arsenal kujiweka pazuri kwenye mchakamchaka wa kutinga hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LONDON, ENGLAND: NDO hivyo. Monaco huenda imegundua ujanja wa kudhibiti mbinu za Arsenal kwenye mipira yao ya kutenga (set-pieces) licha ya miamba hiyo ya Ufaransa kukubali kichapo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika Jumatano iliyopita uwanjani Emirates.

Monaco ilichapwa 3-0 kwenye mchezo huo, Bukayo Saka akifunga mara mbili na Kai Havertz moja. Ushindi huo umeifanya Arsenal kujiweka pazuri kwenye mchakamchaka wa kutinga hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati Arsenal ikiwa na matumaini makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, mambo yanaweza kuwa mabaya kwenye Ligi Kuu England kama timu zitaamua kuiga kilichofanywa na Monaco kwenye kudhibiti mipira ya kona ya Washika Bunduki hao wa London.

Arsenal imekuwa tishio kwelikweli kwenye mipira ya kona, wakipata umaarufu kutokana na kazi nzuri inayofanywa na kocha wao wa mipira ya kutenga Nicolas Jover. Arsenal imefunga mabao 22 kutokana na mipira ya kona kwenye Ligi Kuu England kwa hesabu za kuanzia mwanzoni mwa msimu uliopita.

Lakini, Monaco ilikomesha tishio hilo la Arsenal kwenye mipira ya kona. Wakati Arsenal ilipojiandaa kupiga kona kwenye mchezo huo wa Mabingwa Ulaya, Monaco yenyewe ilibakiza wachezaji watatu mbele. Jambo hilo liliwafanya Arsenal nao kupunguza idadi ya watu kwenye boksi la Monaco na kulazimika kubakiza wachezaji watatu kwenye eneo lao ili kuhakikisha wanadhibiti endapo itatokea shambulizi la kushtukiza.

Na hilo lilionekana kuleta matokeo chanya, kwasababu kipa wa Monaco, Rados-Majecki alikuwa akidaka mipira bila ya kuzongwa.