Monaco kulipa kisasi leo?

Friday November 20 2020
monaco pic

MONACO,UFARANSA. LIGI Kuu Ufaransa inaendelea leo kwa mechi ya kisasi ambapo Monaco ikiwa nyumbani itahitaji kufuta unyonge mbele ya bingwa mtetezi PGS katika mchezo utakaopigwa saa 5:00 usiku.
Monaco inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda michezo miwili ya mwisho ya ligi ambayo imeifanya kushika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 17 huku mpinzani wake PSG katika michezo miwili ya mwisho ikipoteza mmoja wa Uefa na kushinda mmoja wa ligi, ikiwa inashika nafasi ya 11 baada ya kukusanya pointi 24.

Lakini Monaco inaingia ikiwa na rekodi mbaya ya kutopata ushindi katika mechi saba za mwisho ilizocheza dhidi ya PSG ambapo sita ziliisha kwa kupoteza na mmoja ikaambulia sare.

Kiujumla timu hizo zimekutana mara 44 ambapo Monaco ilifanikiwa kushinda michezo 11 na PSG imeshinda 18 huku 15 zikimalizika kwa sare.
Mchezo mwingine utakapigwa katika ligi hiyo leo utakuwa kati ya Rennes ya staa Eduardo na Bordeaux utakaoanza saa 3:00 usiku.

Advertisement