Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Salah mambo ni matamu tu

Muktasari:

  • Salah amekuwa kwenye kiwango bora kabisa msimu huu, akifunga mabao 16 katika michuano yote na kuisaidia Liverpool kuwa vinara kwenye misimamo ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LIVERPOOL, ENGLAND: SUPASTAA, Mohamed Salah amechaguliwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England wa Mwezi Novemba, akifikia rekodi tamu kama mchezaji wa Liverpool.

Salah amekuwa kwenye kiwango bora kabisa msimu huu, akifunga mabao 16 katika michuano yote na kuisaidia Liverpool kuwa vinara kwenye misimamo ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Novemba alionyesha umuhimu wake kwenye kikosi hicho kinachonolewa na kocha Arne Slot.

Fowadi huyo ama amefunga au kuasisti mabao matano kati ya saba yaliyofungwa na Liverpool kwa mwezi huo na miamba hiyo ya Anfield ilishinda mechi zote tatu.

Kiwango chake kilimwingiza kwenye orodha ya wakali wanane waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ya mwezi.

Mo Salah aliibuka kinara kwenye upigaji wa kura za kumpata mshindi na sasa ameungana na wakali Erling Haaland (Agosti), Cole Palmer (Septemba) na Chris Wood wa Nottingham Forest (Oktoba) kwa wachezaji walioshinda tuzo za mwezi kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Mo Salah sasa amefikia rekodi ya Steven Gerrard kwenye idadi ya tuzo za mwezi kwenye Ligi Kuu England kwa upande wa wachezaji wa Liverpool. Wawili hao kila mmoja ameshinda tuzo hiyo mara sita. Lakini, Mo Salah amelingana na gwiji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo kwenye kushinda tuzo ya mwezi mara nane kwenye Ligi Kuu England. Salah alishinda pia Novemba 2017, Februari 2018, Machi 2018, Oktoba 2021 na Oktoba 2023.

Salah sasa anafukuzia rekodi wkenye Ligi Kuu England, ambayo kwa sasa inashikiliwa na wakali wawili, Sergio Aguero na Harry Kane, ambao wameshinda tuzo hiyo ya mwezi mara saba kila mmoja. Kwa maana hiyo, Mo Salah akishinda tuzo mbili tu anaweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi kwenye Ligi Kuu England mara nyingi zaidi ya wengine kwenye historia.