Mo Salah aacha ujumbe mzito kwa Slot, wachezaji
Muktasari:
- Mshambuliaji huyo raia wa Misri pamoja na Andy Robertson wanatarajiwa kuaga rasmi baada ya mechi ya nyumbani dhidi ya Brentford itakayochezwa baadae leo.
LIVERPOOL, ENGLAND: NYOTA wa Liverpool, Mohamed Salah amemtaka Kocha Arne Slot na wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanatwaa ubingwa msimu ujao baada ya mechi yake ya mwisho akiwa na klabu hiyo.
Salah amehitimisha kipindi chake cha miaka tisa Anfield akiwa mmoja wa wafungaji bora zaidi katika historia ya Liverpool baada ya kufunga mabao 255.
Mshambuliaji huyo raia wa Misri pamoja na Andy Robertson wanatarajiwa kuaga rasmi baada ya mechi ya nyumbani dhidi ya Brentford itakayochezwa baadae leo.
“Sitamani kuwa na hisia nyingi leo,” alisema Salah.
“Nashukuru kwa kila dakika niliyokuwa katika klabu hii. Nitachukua kumbukumbu hizi maisha yangu yote.”
Baada ya Robertson kuzungumza, Salah aliongeza ujumbe wa mwisho:
“Kuwa kushinda kwa Liverpool mechi ni jambo bora zaidi linaloweza kukutokea.
“Nafikiri hii ndiyo klabu bora zaidi duniani unaposhinda na mbaya zaidi unapopoteza.
Kwa hiyo hakikisheni mnashinda mwaka ujao na kuchukua makombe.”
Licha ya kuipa Liverpool ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza, Slot amekuwa chini ya presha baada ya timu kufanya vibaya kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na Ligi Kuu England.
Wiki iliyopita Salah alizua mjadala baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii uliotafsiriwa ni ukosoaji kwa Slot, akitaka Liverpool kurejea kwenye mfumo wa “heavy metal football” uliokuwa chini ya Jurgen Klopp.
Slot alisema ataendelea kumkumbuka Salah kama mashine ya mabao aliyesaidia timu kutwaa mataji muhimu.
“Asilimia 100, ubingwa wa Ligi Kuu England wa msimu uliopita ndiyo mafanikio makubwa zaidi maishani mwangu na Salah alikuwa muhimu sana kwa hilo,” alisema Slot.
Salah anatoka Liverpool akiwa amechukua ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja, huku akicheza michezo 441 na kufunga mabao 257