Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi Barcelona apotezea usajili wa Lionel Messi

DECO Pict

Muktasari:

  • Messi amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kurudi Barcelona, klabu ambayo aliitumikia kwa zaidi ya miaka 15 kwa mafanikio makubwa. 

Mkurugenzi wa Barcelona, Deco, amebainisha kuwa hawezi kusema kama klabu hiyo inaweza kumsajili nahodha na mshambuliaji wa Inter Miami, Lionel Messi, kwa mkopo wa muda mfupi.

Messi amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kurudi Barcelona, klabu ambayo aliitumikia kwa zaidi ya miaka 15 kwa mafanikio makubwa. 

Deco amesema ni suala gumu kwa sasa kueleza uwezekano wa kumsajili Messi kwa mkopo wa muda mfupi, kutokana na mkataba wake na Inter Miami inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani.

Amesema Barca inatamani kuwa na mchezjai kama Messi katika kipindi hiki ambacho wapo kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu La Liga, lakini kwa sasa hawezi kutoa uhakika wowote kwa mashabiki kama mpango huo unawezekana ama la.

“Leo Messi kwa mkopo wa muda mfupi? Sidhani kuwa hiyo inawezekana. Leo ana mkataba. Sidhani kama suala hili limewahi kuibuliwa… Messi daima ni Messi, daima anaweza kuleta kitu kwenye kikosi chetu, lakini si jambo ambalo tutaongea kuhusu sasa hivi,” amesema Deco.

DEC 01
DEC 01

Mshambuliaji huyo wa Argentina, aliachana na Barcelona mwaka 2021 na kujiunga na Paris Saint-Germain kwa usajili huru, hali ambayo iliacha majonzi kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo ya Catalunya.

Baadaye, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, aliondoka PSG na kujiunga na klabu ya Major League Soccer (MLS), Inter Miami.

Lionel Messi amejenga historia kubwa duniani katika soka la ngazi ya klabu. Akiwa na Barcelona, alifunga mabao 672 katika michezo 778, akiwa moja ya washambuliaji bora zaidi. 

Baada ya kuondoka Barcelona mwaka 2021, Messi alijiunga na Paris Saint‑Germain (PSG) na kufunga mabao 32 katika michezo 75. 

Kwa sasa, yupo Inter Miami, amefunga mabao 77 katika takriban mechi 87, akionyesha bado ana uwezo wa kipekee anapokuwa uwanjani. Takwimu hizi zinathibitisha jinsi Messi ni mchezaji muhimu, akitoa mchango mkubwa kwa kila klabu anayoichezea.