Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkataba unamsubiri Silva Benfica

Muktasari:

  • Akizungumza kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, Lopes alidai kuwa mkataba tayari “unasubiri” kwa ajili ya nyota huyo wa Ureno, ambaye bado yuko chini ya mkataba na Man City hadi mwisho wa msimu huu ingawa anaweza kuruhusiwa kuondoka mapema Januari.

LISBON, URENO: MGOMBEA urais wa Benfica, Joao Noronha Lopes, ameweka wazi mpango wake mkubwa wa kumrejesha Bernardo Silva katika klabu yake ya utotoni akitokea Manchester City.

Akizungumza kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, Lopes alidai kuwa mkataba tayari “unasubiri” kwa ajili ya nyota huyo wa Ureno, ambaye bado yuko chini ya mkataba na Man City hadi mwisho wa msimu huu ingawa anaweza kuruhusiwa kuondoka mapema Januari.

Lopes, ambaye anawania urais wa Benfica katika uchaguzi wa Oktoba 25, ameweka ahadi ya kumrejesha Silva kwenye timu hiyo kama kiini cha kampeni yake.

Vilevile, ametoa mpango wa kufanya mazungumzo na Manchester City Januari, ingawa uwezekano wa usajili kufanyika majira ya kiangazi pia upo kutokana na mkataba wa Silva kuisha 2026.

Akizungumza na gazeti la A Bola la nchini Ureno, Lopes alisema: “Ndiyo, naweza kuthibitisha kuwa kuna mkataba unamsubiri Bernardo Silva. Na ninataka sana kumleta Januari. Yeye anawakilisha kila kitu ninachokitaka kwa Benfica: utambulisho, utamaduni wa ushindi, na ni shabiki halisi wa Benfica. Na naweza kuwahakikishia kuwa hatutaishia hapo kwake pekee.”

Silva, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31, alipitia katika akademi ya Benfica kabla ya kwenda Monaco kwa mkopo mwaka 2014 kisha baadaye kusaini mkataba wa moja kwa moja.

Kiungo huyo amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na kurejea Lisbon, ambako bado anapendwa sana na mashabiki wa Benfica.

Licha ya kusaini mkataba mpya na Manchester City mwaka 2023, tetesi kuhusu mustakabali wake zimeendelea kuibuka mara kwa mara.

Ahadi ya Lopes inaweza kuwa silaha kubwa ya kisiasa katika kampeni, japokuwa kuishawishi Man City imuachie Silva katikati ya msimu huu huenda ikawa ngumu.

Uchaguzi wa urais wa Benfica utafanyika Oktoba 25, na ahadi ya Lopes huenda ikawavutia wapiga kura wanaotamani kumuona Silva akirejea. Ikiwa atachaguliwa, mazungumzo na Manchester City yataanza mara moja.