Mkali Osimhen aipeleka Nigeria nusu fainali Afcon 2025
Muktasari:
- Nigeria ilikuwa imara katika kipindi cha kwanza huko Marrakech, huku Adams akikosa nafasi ya kufunga dakika nane kabla ya mapumziko baada ya mpira wake kupita pembeni ya lango.
MARRAKECH, MOROCCO: VICTOR Osimhen na Akor Adams wameunga mabao muhimu kupeleka Nigeria hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baada ya kuichapa Algeria mabao 2-0.
Nigeria ilikuwa imara katika kipindi cha kwanza huko Marrakech, huku Adams akikosa nafasi ya kufunga dakika nane kabla ya mapumziko baada ya mpira wake kupita pembeni ya lango.
Osimhen alivunja ugumu wa Algeria katika kipindi cha pili baada kupokea pasi ya Bruno Onyemaechi kutoka upande wa kushoto na kuifunga Algeria bao la kwanza. Adams aliongeza bao la pili dakika 10 baadaye baada ya Osimhen kumtengenezea nafasi ya kufunga.
Nigeria, walikuwa wa pili mwaka 2023, sasa watakabiliana na wenyeji Morocco katika nusu fainali mjini Rabat siku ya Jumatano.