Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mjipange! Spurs ikinunuliwa tu, vyuma vinatua

SPURS Pict

Muktasari:

  • Tovuti ya The Sun imefichua kundi la wafanyabiashara kutoka Marekani limewasilisha ofa ya kuinunua timu hiyo ya London wakiongozwa na tajiri Brooklyn Earick.

LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM huenda ikashusha mastaa wakubwa na kujenga timu imara ikiwa mpango wa kununuliwa na moja kati ya kampuni za Marekani utakamilika.

Tovuti ya The Sun imefichua kundi la wafanyabiashara kutoka Marekani limewasilisha ofa ya kuinunua timu hiyo ya London wakiongozwa na tajiri Brooklyn Earick.

Matajiri hao 12, ambao wanamiliki timu za NFL na NBA wapo tayari kutoa Pauni 3.3 bilioni kama pesa ya kuinunua Spurs kisha Pauni 1.2 bilioni itaweka kama sehemu ya ada ya kusajili wachezaji pamoja na malipo ya mishahara na mawakala.

Kwa sasa Spurs ipo katika hali nzuri kwenye upande wa ununuzi na matumizi, hivyo, ikiwa matajiri hao pia wataweka pesa itakuwa na uhuru wa kusajili wachezaji wengi wa bei ghali bila ya kuvunja sheria.

Wachezaji wapya ghali sita wanaweza kutua katika viunga hivyo kuanzia kwa Marc Guehi ambaye mkataba wake na Crystal Palace unamalizika mwisho wa msimu na anawindwa na Liverpool lakini kwa mpunga ambao Spurs watakuwa nao wataweza kumshawishi kwa mshahara mnono na kumpata bila shida.

Kwenye eneo la katikati ya uwanja, vijana hawa wa London wanaweza kuipata huduma ya Frenkie de Jong wa Barcelona ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu na ikiwa itawasilisha ofa nono anaweza kushawishika na mastaa kama Vinicius Jr ambaye hana furaha kwa sasa katika kikosi cha Real Madrid anaweza kutua Spurs hata kwa mkataba wa muda mfupi.

Ikiwa matajiri hao watachukua timu, uwezekano wa Harry Kane kurudi pia unatajwa kwani ana kipengele ambacho kinaeleza anaweza kuachiwa mwisho wa msimu kwa kiasi kisichozidi Pauni 50 milioni lakini kwa sharti la kutoa taarifa ya kuondoka Januari mwakani.

Kwa sasa wamiliki wa Spurs ni kampuni ya ENIC Group ambayo ina asilimia 86, huku asilimia zilizosalia  zikimilikiwa na watu wengine.